Wasichana watakiwa kujiunga na vyuo vya misitu kupata ajira za uhakika

Mkufunzi wa Chuo cha Misitu cha Olmotonyi, Arusha, Philipina Shayo akizungumza na mmoja wa wadau wa misitu, mwishoni mwa wiki jijini Dar es ... thumbnail 1 summary
Mkufunzi wa Chuo cha Misitu cha Olmotonyi, Arusha, Philipina Shayo akizungumza na mmoja wa wadau wa misitu, mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 

Wito umetolewa kwa wanafunzi wa kike nchini kujiunga na vyuo vya misiti nchini na kuachana na dhana kuwa vyuo hivyo ni kwajili ya wanaume kwa kuwa ajira zake nyingi ziko vijijini.


Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkufunzi wa Chuo cha Misitu cha Olmotonyi, Arusha, Philipina Shayo katika mahojiano maalumu na www.tabianchi.blogspot.com jijini Dar es Salaam.

Shayo alisema kuwa wasichana wengi hawapendi kujiunga na vyuo vya misitu kwa kuhofia ajira zao kuwa vijijini na hivyo kuona kama watakosa raha na starehe za mijini.

“Dhana hiyo ya wasichana ya kudhani kuwa watu wanaosoma vyuo vya misitu watapata ajira maporini, wanapaswa kuachana nayo, nawashauri wajiunge na vyuo hivi halafu wataona matunda yake” alisema Shayo.

Alisema kuwa kwa hali ya maisha ilivyo sasa hawapaswi kuchagua kazi wala vyuo vya kusoma kwa kuwa vyuo vya misitu ni moja ya maeneo ambayo yanatoa ajira za kudumu na zenye maslahi makubwa.
Shayo alisema kuwa chuo chake kinamazingira mazuri ambayo yatamwezesha mwanafunzi hasa wa kike kusoma bila shida na kujipatia elimu yake ya misitu ambayo itamwezesha kulisaidia taifa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumzia mwamko wa wanafunzi kujiunga na masomo katika chuo hicho, Shayo alisema idadi ya wanafunzi wanaojiunga chuoni hapo imeongezeka mwaka huu ukilinganisha na miaka  mitano iliyopita.