Vodacom yazindua tuzo za Blogs na website nchini

Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania leo imezindua tuzo ilizozipa jina la ‘Vodacom Award of Digital Excellence’. Katika tuz... thumbnail 1 summary
Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania leo imezindua tuzo ilizozipa jina la ‘Vodacom Award of Digital Excellence’.

Katika tuzo hizo blogs na website kumi bora nchini zitatuzwa kutokana na juhudi na mafanikio yake, jambo ambalo ni la kwanza kufanywa na Vodacom Tanzania.

Hiyo itakuwa tuzo na mpango wa ushirikiano ambao ni kama dalili ya mtandao huo kujitahidi katika kuendeleza sekta ya habari za kidigitali nchini.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, amesema Vodacom inauona uchapishaji, uzalishaji na mawasiliano ya digitali kama kitu muhimu katika kuiendeleza jamii.

“Ni matumaini yetu kwamba kwa kuzindua tuzo hizo na mpango wa ushirikiano tutaweza kuwa na mchango katika kipindi hiki cha sekta ya digitali nchini Tanzania. Katika mpango huu tutawaangaza watu waliopo kwenye technolojia mahsusi ya digitali na kuwapa tuzo, kuwasaidia na kuwaongeza ujuzi,” alisema Meza.


Rene Meza (Managing Director - Vodacom Tanzania
“Hiyo ndio sababu ya sisi kuwatuza kwa jitihada na mabadiliko waliyoyaleta.”

Washirika wa kuanzia kwenye kigezo cha Blog/Website walichaguliwa kwa kutajwa katika mchakato wa siri uliofanywa na wataalam katika midani ya technlojia nchini.

Ili kufuzu kutajwa kama mshirika wa mpango huo, watajwa wanatakiwa kukidhi vigezo vikiwemo: Kupromote uundwaji wa vitu/content halisia, kuzingatia sheria za vyombo huru na kuonesha dalili za kukua siku za usoni.

Watajwa wa siku za baadaye watakuwa wakitajwa katika mchakato wa wazi.
Pamoja na vigezo hivyo, ili watu/mtu aweze kupewa tuzo ni lazima aoneshe usomwaji wa uhakika wa vyombo vyao.

Vodacom itawatangaza washirika wa kwanza wiki ijayo na imeahidi kuviangaza vipaji bora zaidi kwenye tasnia ya digitali nchini.
 
Chanzo: Leotaiment blog