Hifadhi ya kisiwa cha Saanane, ilianzisha kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania 1964. Lengo la kuanzishwa kwa hifadhi hii ya...
13:17
Hifadhi ya kisiwa cha Saanane, ilianzisha kama bustani
ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania 1964. Lengo la kuanzishwa kwa hifadhi hii
ya Saanane ilikuwa ni kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii.
Jina la hifadhi
ya Saanane lilitokana na muanzilishi ya bustani alieitwa Saanane Chawandi, kati
ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali wahihamishiwa katika kisiwa hiki ni
pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia,
kima, twiga, nungunungu, mamba, simba, nyoka .n.k Wanyama wakali kama faru na
mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachiwa huru. Bustani hii iligeuzwa kuwa
pori la akiba (game reserve) mwaka 1991.
Muonekano wa Ziwa Victoria kutoka katika kisiwa cha
Saanane iwapo jijini Mwanza ni kivutio kikubwa sana , Hifadhi hii inaeneo la
mita za mraba 0.5, na iko umbali wa km 2 kusini magharibi kutoka katikati ya
jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria. Kisiwa cha Saanane
kinafikiwa
kwa boti ukitokea jijini Mwanza. Mtu anaweza kufika jijini Mwanza kwa
gari,ndege, treni,mguu na kwa boti.Shunguli za kufanya hifadhini Saanane ni
pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, na safari za
kutembea, kupiga makasia kwa kutumia boti, Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha
Saanane inapitika wakati wote wa mwaka. kwa wanaotarajia kutembea kisiwa cha
Sanane kujua garama wasiliana na:
KISIWA CHA SAANANE
S.L.P 11775,Mwanza
simu:+255 28 2541819
barua pepe: saanane@tanzaniaparks.com