Oparesheni ya kukamata majangili Wilayani
Liwale Mkoani Lindi imezaa matunda baada ya kufanikiwa kukamata watu 101 wakiwa
na nyara za serikali zenye thamani ya sh.212.9 milioni.
Taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki inaeleza kuwa kati ya watuhumiwa
hao tayari kesi 15 zimeshafikishwa mahakamani na moja imeshatolewa hukumu huku
kesi nyingine zikiwa katika utaratibu wa kufikishwa mahakani.
Kagasheki alitaja nyara zilizokamatwa
kuwa ni pamoja na meno 80 ya kiboko yenye thamani ya sh. 18.8 milioni, meno 14
ya tembo yenye thamani ya sh. 164 milioni na bangili moja ya usinga wa mkia wa
tembo yenye thamani ya sh. 23.6 milioni.
Nyara nyingine zilizokamatwa ni ngozi
mbili za samba zenye thamani y ash.15.4 milioni, ngozi ya chui sh.5.5 milioni,
mikia miwili ya ngedere sh. 378,000, kichwa cha nyati chenye mapembe sh.2.6
milioni na kichwa cha pofu chenye thamani ya sh.2.6 milioni.
Kagasheki alisema mbali na kukamata nyara
hizo pia wanashikilia mali za majangiri na vifaa vya ujangili ikiwemo gari aina
ya Toyota corona yenye namba za usajili T836 ADV, pikipiki mbili aina ya Sanlg
zenye namba za usajili T901 BXQ na T772 BSD, msumeno wa kuchania mbao na mbao
149.
Tabianchi