UNAVYOWEZA KUTUMIA ASALI KAMA TIBA YA KUACHA KUKOJOA KITANDANI KWA MWANAO

Wengi tushawahi kuusikia wimbo maarufu na pengine mfupi kuliko yote mitaani kwetu katika enzi za ukuaji wetu, wimbo huu ulikuwa unaimbwa hi... thumbnail 1 summary
Wengi tushawahi kuusikia wimbo maarufu na pengine mfupi kuliko yote mitaani kwetu katika enzi za ukuaji wetu, wimbo huu ulikuwa unaimbwa hivi:-
“Kikojozi na nguo kaitia moto na ndani ina viroboto huyo” 

Wimbo huu unapoimbwa mtoto kikojozi hutangulizwa mbele na watoto mbalimbali humfuata kwa nyuma huku wakipiga vyombo mbalimbali vinavyotoa mdundo usio rasmi; yote hiyo ni kutaka kumfedhehesha mtoto anayekojoa kitandani ili aepukane na tabia hiyo. 

Lakini kwanini mwanao afedheheke mtaani? Na pengine kuathirika kisaikolojia wakati tuna maliasili zakutosha nchini na zinazopatikan kirahisi?
Sasa ni wakati wako wewe mzazi kumnuthuru mwanao na tabia ya kukojoa kitandani kwa kumlisha asali kiasi cha kijiko kimoja cha chai kabla hajaenda kulala, asali inazuia maji kutoka mwilini, na hivyo mtoto atapunguza kukojoa au kuacha kabisa!


TAFADHALI MJULISHE NA MZAZI MWENZAKO MARA BADA YA KUSOMA HABARI HII!!!
Chanzo: Maliasili zetu