Umewahi kujiuliza
majangili wanaojihusisha na kuua tembo (na wakati mwingine kuua askari
wanayampori) huwa wanapatiwa adhabu gani? Adhabu hizo zinatosha ukilinganisha
na uharibifu mkubwa wanaoufanya na kulipotezea taifa mapato na nguvu kazi yake.
Kupitia majadiliano ya pamoja ya wadau mbalimbali waliohudhuria siku ya tembo kitaifa yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam Septemba 22, 2013 wamependekeza adhabu kali kwa majangili zitungwe.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa
Wadau wa mambo ya utalii wakifuatilia mada wakati wa maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa
Katika kipengele kimoja
wapo cha mapendekezo hayo kinapendekeza sheria za wanyamapori zijadiliwe upya
na bunge na kuingizwa kipengele kitakachoruhusu majangili kuuawa.
Yafuatayo ni
mapendekezo 14 ya pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali wa utalii ambayo kwayo
tunaweza kukomesha ujangili Tanzania
1. Sheria
ziwe kali. Wabunge wajadili upya sheria ya wanayamapori ikiwezekana sheria ya kuua
majangili iruhusiwe.
2. Mh.
Rais apewe taarifa kuhusu hali halisi ya ujangili wa tembo na atangaze kuwa
hili ni janga la kitaifa hivyo abariki Operation Uhai irudi tena. Pia atoe
agizo kwa jeshi lisaidie katika kupambana na ujangili wa tembo
3. Ushirikishwaji
wa jamii ni muhimu katika mapambano dhidi ya ujangili wa tembo
4. Idara
ya wanyamapori iongezewe nguvu za kifedha na rasilimali watu
5. Mahitaji
makubwa ya matumizi ya teknolojia katika kuhifadhi tembo
6. Kupambanua
na kubainisha aina ya majangili wa tembo waliopo nchini na njia za kukabiliana
nao
7. Bandari
zetu zinatakiwa ziwezeshwe kuwa na vifaa vya kubaini meno ya tembo na hata
bidhaa zingine wakati zinatoka Tanzania kwenda nchi nyingine. Maana utaratibu
wa sasa ukaguzi unafanywa kwenye mizigo inayoingia ndani ya nchi pekee
8. Ushirikishwaji
wa waandishi wa habari upewe kipaumbele ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kifedha
na kitaaluma ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa
9.
WMAs zilizopo ziwezeshwe na
ikiwezekana zianzishwe nchi nzima
10.
Ushirikishwaji wa wadau mbalimbali
katika utafiti wa tembo
11.
Kama mwanachama wa CITES, Tanzania
iombe kuwa na mkutano wa wadau wote na kuomba kuwa na ajenda ya kusitisha
kabisa biashara ya meno ya tembo
12.
Kuwepo na jukwaa la pamoja katika
kupambana na ujangili wa tembo. Ili wadau wakutane wote kupeana taarifa na
kupanga mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ujangili
14.
IRA kuandaa siku ya tembo kitaifa,
mwaka 2014
Endapo mambo haya yakizingatiwa yanaweza kuleta
mabadiliko na kupunguza kasi ya ujangili nchini, nap engine ni wakati sasa kwa
Rais kuchukua hatua kunusuru tembo wetu na wanyama wengine ambao wako hatarini
kutoweka.
Maandhimisho ya siku ya tembo kitaifa,
yaliandaliwa na taasisi ya tathmini ya rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wataalamu wa mambo
ya mazingira na utalii kutoka UDSM, wanafunzi, wanachuo, waandishi wa habari na
wadau mbalimbali kwa ujumla wake.
Taasisi hiyo ya Tathmini ya Rasilimali Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (IRA) imepewa tena jukumu la kuwa mwandaaji mkuu wa siku ya
tembo kitaifa mwaka 2014
www.tabianchi.blogspot.com