Confirmed: Safari ya fastjet kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg kuanza rasmi Ijumaa Octoba 18, 2013

Wiki chache zililozipa kulitokea wingu zito na sintofahamu ya lini Safari ya kwenza ya kimataifa ya fastjet kati ya Dar es Salaam kwenda ... thumbnail 1 summary
fastjet's first international flights ready for take off!
Wiki chache zililozipa kulitokea wingu zito na sintofahamu ya lini Safari ya kwenza ya kimataifa ya fastjet kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini baada ya safari hiyo kuahirishwa kutokana na sababu kadhaa zilizoelezwa na fastjet.

Lakini sasa imekuwa confirmed kwamba safari hiyo ya kwanza ya kimataifa ambayo awali ilipangwa kufanyika septemba 27 mwaka huu sasa itafanyika Octoba 18 yaani ijumaa ya wiki hii.

CEO wa Fastjet na Interim Chairman Ed Winter amesema kuwa:
"Idara ya uchukuzi ya Afrika Kusini imekamilisha upitiaji wa documents zetu  za ziada walizotuomba na kutoa kibali cha kufanya kazi zetu, na sisi kwa kuona hivyo tumeamua kuendelea na ratiba yetu ya safari hii mpya"
"Hadi wakati huu safari za ndege kati ya Dar es Salaam na Johannesburg bado ni za gharama ya juu sana, kuzinduliwa kwa safari yetu kutawasaidia watu wengi kutokana na kuwa na bei nafuu na huduma za uhakika" anaeleza Winter.
Katika taarifa hiyo fastjet wameonyesha furaha ya kuanza kwa safari yake ya kimataifa ikiwa ni hatua kubwa ya kuelekea kule wanakokuita kwenye mafanikio na kuwahudumia watu wengi kwa gharama nafuu.

Safari hiyo ya kwanza itafanyika siku ya ijumaa ambapo ndege itaondoka kwenye Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:15 asubuhi na kufika kwenye Uwanja wa kimataifa wa O.R. Tambo Afrika Kusini majira ya saa 5:45 asubuhi.

Fastjet itakuwa ikifanya safari zake katika ya Dar es Salaam na Johannesburg mara tatu kwa wiki, siku za jumatatu, jumatano na ijumaa na huenda safari hizo zikaongezeka kutegemeana na ongezeko la abiria.

Nauli ya safari hii ni 160,000TSh kwa safari moja bila VAT, zaidi tembelea www.fastjet.com


tabianchi