Si mara moja kukuta mtu akichanganya kati ya wanyama hawa wawili, Chui na Duma (Cheetah) anapowaona kwenye hifadhi mbalimbali hapa nchini. leo nimeona nilete kwako tofauti zako ili usiendelee kuwachanganya tena. Kupitia picha na maelezo machache yafutayo utaweza kujifunza kitu.
Chui, naamini kabisa kwa kuangalia picha hii unaweza kubaini alama katika madoa yake mwilini
Picha hii pia inatosha kubaini madoa ya duma na umbo lake.
Dondoo:
Chui anaumbo nene na lenye ukakamavu, kwa kuwa ameumbwa kutumia nguvu zaidi katika shughuli zake wakati Duma anaumbo jembamba na refu kwa ajili ya kasi kubwa wakati wa kukimbia.
Chui hufanya mawindo yake nyakati za usiku zaidi wakati Duma yeye huona vizuri zaidi mchana kuliko usiku hivyo uwindaji kwake ni mchana zaidi.
Uso wa chui
Chui
ni mnyama mwindaji anayewinda kimyakimya sana. Ingawa ni mdogo kuliko wanyama
wote wa jenasi ya Panthera, chui bado anaweza kuwinda mnyama mkubwa kwasababu
ya fuvu lake kubwa lenye taya zenye nguvu.
Ukilinganisha
na paka mwili wake ni mrefu zaidi na miguu mifupi na minene, Urefu wa kichwa na
mwili wake ni kati ya sm 125 na 165 na mkia wake unakaribia sm 60 mpaka 110.
Urefu
wa mabega ni sm 45 mpaka 80. Chui dume ni wakubwa 30% zaidi ukilinganisha na
jike, kufikia uzito wa kg 37 mpaka 91 ukilinganisha na jike wenye kg 28 mpaka
60.
Madoa
ya chui ni ya mviringo kwa Afrika Mashiriki na huwa ya mraba kwa kusini mwa
Afrika wakati chui ana madoa ndani ya miduara midogo kuliko ile ya duma.
Chui ni mkubwa na mwenye misuli zaidi kuliko duma.
Chui
anafahamika kwa uwezo wake wa kukwea miti, na huonekana akijipumzisha kwenye
matawi ya miti wakati wa mchana, akiburuza mawindo yake mpaka juu ya miti na
kuining’iniza huko; ingawa, yeye hana nguvu sana kama jamii nyingine ya paka.
Chui
naye pia ni mwenye nguvu sana, anaweza kukimbia mpaka km 58 kwa saa, kuruka
mbele zaidi ya mita 6 na kuruka juu mpaka kufikia hata mita 3. Chui kiasili ni miongoni mwa
wanyama wanaowinda usiku, japo wamerekodiwa mara kadhaa wakiwinda mchana, tena
hasa wakati anga likiwa si angavu sana. Wao hutumia muda wao mwingi kulala,
aidha juu ya miti, kwenye miamba au kwenye nyasi.
Chui
huwinda kwa utegemezi. Ingawa hupendelea wanyama wa umbo la kati, chui hula
kitu chochote kuanzia kombamwiko alaye kinyesi mpaka wakubwa pofu dume mwenye
kg 900. Milo yao hujumuisha sana wanyama wenye kwato na nyani, lakini rodent,
reptilia, amfibia, ndege na samaki nao huliwa pia. Kwa Afrika, swala wa umbo la
kati ndio chakula kikuu cha chui, hasa impala na swala wa Thomson.
Chui hunyatia windo lake kimyakimya na dakika ya mwisho kisha kumrukia,
humnyonga koo lake kwa kumng’ata haraka. Chui kwa kawaida huficha mawindo yao
kwenye vichaka vilivyoshona au huyachukua mpaka juu ya miti, na wana uwezo wa
kubeba wanyama hata wenye uzito mara tatu ya uzito wao.
Chui ndiyo mnyama pekee
miongoni mwa jamii ya paka anayeweza kubeba mawindo yake juu ya miti. Uchaguzi
wa mawindo kupitia tafiti umeonekana kuzingatia hali fulani ikiwemo ukubwa wa
kundi analokuwemo mnyama awindwaye, ukubwa wa pori na mazingira yasiyoweza
kuhatarisha maisha ya mwindaji, chui.
Uso wa Duma
Duma ni mnyama katika kundi la wanyama walao nyama, yuko katika jamii
ya paka. Ngozi yake ni
manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi.
Kichwa
chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama
chui. Wanapokua, madume hutembea peke yao katika kundi
duma watatu au wawili.
Wanaungana
na majike wanapokuwa kwenye joto tu na sivinginevyo. Rangi ya duma
inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona
ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia
katika mawindo yao.
Ndiye
mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao
kwa miguu hukimbia kilometa 113 kwa saa. Chakula chake ni wanyama jamii ya
swala hupatika Afrika na kidogo sehemu za Asia.
Tabianchi