JK AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA ANGA (ICAO) IKULU JIJINI DAR

Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la  Anga (ICAO) Raymond Benjamin Ikulu jijini Dar es Salaam,... thumbnail 1 summary
Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la  Anga (ICAO) Raymond Benjamin Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu huyo yupo nchini kwa ziara ya Kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete akiongea na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la  Anga (ICAO) Raymond Benjamin, wakati alipofika Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu huyo yupo nchini kwa ziara ya Kikazi kuanzia Mei 14 hadi 18 Mei 2014.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Anga (ICAO) Raymond Benjamin, wakati alipofika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ziara ya Kikazi kuanzia Mei 14 hadi 18 Mei 2014.Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, pamoja na viongozi wakuu wa TCAA.
Rais Jakaya Kikwete akiagana na mgeni wake Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la  Anga (ICAO) Raymond Benjamin, baada ya kumalizika kwa maongezi yao ya kikazi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baaddhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA wakati walipokuwa katika ziara ya kikazi na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin ambaye yupo nchini kuanzia Mei 14 hadi Mei 18 2014.Tanzania ni miongoni mwa nchi 24 za ESAF zilizoko Kusini Mashariki mwa Afrika na Majukumu yake ni Pamoja na Kuendeleza sere,Maamuzi , Kanuni na Mapendekezo,Mipango ya uendeshaji wa sekta Usafiri wa anga inayoratibiwa na ICAO, Pamoja na kutoa misaada ya Kiufundi.