MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI TAREHE 0 1- 05 JUNI, 2014, KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Ernest Ndikilo akiongea na wanahabari  Mkuu wa Mkoa wa Mwaza anapenda kuwafahamisha ya kwamba, siku ... thumbnail 1 summary
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Mhe. Ernest Ndikilo akiongea na wanahabari 
Mkuu wa Mkoa wa Mwaza anapenda kuwafahamisha ya kwamba, siku ya madhimisho ya mazingira Duniani, hufanyika kuanzia  tarehe 01 hadi 05 ya mwezi Juni, kwa  kila Mwaka. Kwa mwaka 2014 shirika la Umoja wa mataifa linalo shughulikia mazingira limetangaza  Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni “RAISE YOUR VOICE BUT NOT THE SEAL  LEVEL” kwa tafsiri ni “CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA TABIANCHI na kitaifa” TUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MBADILIKO YA TABIANCHI.

Kwa mwaka huu wa 2014 Mkoa wetu wa  Mwanza umeteuliwa kuwa mwenyeji wa kitaifa, kwa  wiki ya maadhimisho ya Mazingira Duniani, ambapo katika juma hilo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira  kwa njia ya Makongamano, kupanda miti, kuzoa takataka, maonesho ya utunzaji na mazingira, kuondoa magugu katika Ziwa Victoria na ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara kwenye maeneo tofauti yanayo jishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.
 Ufungunguzi wa maadhimisho kitaifa utafanyika tarehe 02 Juni, 2014 kuanzia saa 1.00 asubuhi katika Viwanja vya Furahisha na siku ya kilele itakuwa tarehe 05 Juni, 2014 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
 Shughuli zitakazo fanyika siku hiyo ni pamoja na-; kukabidhi vyeti kwa wadau mbali mbali wa mazingira, zawadi na tuzo za utunzaji uhifadhi wa mazingira pamoja na zawadi kwa washindi wa wa kuhifadhi mazingira.
 Aidha  Mkoa unategemea kupokea Wageni wa Kitaifa na  Kimataifa, Aidha Viongozi wa Kitaifa watatembelea Makampuni na kuona utunzaji wa Mazingira na jinsi ya kutenga taka ngumu na zisizo ngumu.
 Nichukue fursa hii kutoa rai kwenu kuwa “ ukitaka kuona mgeni anafurahia makaribisho yako ukarimu ni kitu muhimu sana, Nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kuwalaki wageni wote watakao tufikia katika juma zima hilo lakini pia kama ilivyo desturi yetu wanamwanza tuonyeshe ukarimu kwa wageni wetu na pindi waondokapo basi waikumbuke Mwanza.

“TUNZA MAZINGIRA, KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI”
IMETOLEWA NA MKUU 
WA MKOA WA MWANZA.