Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
Zaidi
ya machifu 100 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia
kushiriki katika tamasha la "Mtu Kwao" linalotarajiwa kuanza kutimua
vumbi May 15 hadi 20 mwaka huu katika kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri
Abeid jijini hapa.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini hapa Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni
mkurenzi wa kampuni ya Utamaduni Traning L.T.D Janeth Jonas alisema
kuwa tamasha hilo litashirikisha machifu 120 kutoka katika mikoa
mbalimbali na makabila mbalimbali ya hapa nchini.
Alibainisha
kuwa nia na dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni
kuweza kuuenzi utamaduni wa mtanzani ambapo ni kuanzia mavazi ya
makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma kutoka katika makabila yote
hapa nchini.
“Pia
katika tamasha hili tumeamua kuwaita machifu mbalimbali l kutoka katika
makabila mbalimbali hapa nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria
ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha
kwaajili ya tamasha hili Gerald Mandera ,chifu Gilbert Rugal Isambe
kutok a kasulu na wengine wengi wote watakuwepo”alisema Janeth
Aidha
alisema kuwa katika tamasha hili kila mtu atapata fursa ya kuona ngoma
kutoka katika makabila mbalimbali pamoja na kuonja chakula cha kila
aina cha makabila ya hapa nchini pamoja na nje ya nchi
Alisema
kuwa pia katika tamasha hili zaidi ya vikundi vya ngoma 100
vitatumbuiza pamoja na wasanii mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za
utamaduni Mrisho mpoto, Wema Sepetu, kundi la Weusi kutoka Arusha, Jambo
Squard, Dogo Janja pamoja na msanii kutoka nchini Kenya Daniel ole
Sekuo.
Naye
mmoja wa machifu ambaye atahudhuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera
kutoka Old Moshi alisema kuwa waandaaji wamefanya jambo jema sana
kuanda tamasha hili kwani wao ndio wametambua uwepo wa machifu na
wameona umuhimu wao mpaka wameamua kuwakusanya pamoja katika tamasha
kama hili.
Alisema
kuwa sasa hivi serikali nayo inawajibu wa kujipanga vilivyo na kutenga
siku maalumu kwa ajili ya kufanya tamasha hili kama jinsi wenzetu kutoka
katika nchi zingine wanavyo azimisha siku hii katika tarehe hizi na
mwezi huu kila mwaka.
Aidha
alibainisha kuwa kuwakusanya watu mbalimbali kutoka katika tamaduni
mbalimbali pamoja na makabila mbalimbali itasaidia kwani inaweza
kuwezesha hata nchi kupata vazi la taifa kwani makabila haya yate
yanakuja yakiwa yamevaa vazi la ukabila wao na hii itakuwa fursa pekee
ya kuweza kuchagua vazi hasili la mtanzanzia.
“Ni
aibu kubwa sana unakuta sisi kama Watanzania hadi leo hii hatuna vazi
linaloweza kutuwakilisha sisi kama Watanzania na ukiangalia wenzetu wa n
je ya nchi wanamav azi yao ya kiutamaduni ambao ukimuona tu mtu amevaa
unajua katoka katika kabila Fulani ,naitanishangaza sana kuona mtu
anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele utamaduni wa kigeni “alisema
chifu Gilbert Isambe akibainisha kuwa hii ni fursa ya watu kuja
kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo
Chifu Gilbert Isambe akiwa na vazi la
kichifu
Chifu Gilbert Isambe akiongea na vyombo vya habari. Pembeni yake ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao Bi. Janeth Jonas