MANTRA YASAINI MAKUBALIANO NA SERIKALI KUPIGA VITA UJANGILI WA NDOVU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Chris Sattler, Afisa Mtendaji Mkuu wa Uranium One, (wa pili kushoto) waki... thumbnail 1 summary


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Chris Sattler, Afisa Mtendaji Mkuu wa Uranium One, (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambao inairuhusu kampuni ya uchimbaji madini ya urani ya Mantra Tanzania kuwekeza dola za Kimarekani 800,000 katika mwaka 2014 itakayo tumika katika shughuli za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyanya nchini Tanzania. Aliyesimama ni Galina Molchanova, Makamu wa Rais wa kamapuni ya Mantra Tanzania. Hafla hiyo fupi ilifanyika sambamba na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
=========  ========
Mantra yasaini makubaliano na Serikali kupiga vita ujangili wa ndovu
·         Yawekeza dola za kimarekani 800,000 mwaka 2014 katika vita dhidi ya ujangili.

Dar es Salaam, Tanzania – KAMPUNI ya Mantra Tanzania na Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Wildlife Division) wamesaini mkataba wa makubaliano, ambao umelenga kwa pande zote mbili kushirikiana katika kupiga vita ujangili wa tembo katika eneo la kusini mwa hifadhi ya wanyamapori ya Selous. Katika makubaliano hayo, kampuni ya Mantra Tanzania itawekeza Dola za Kimarekani laki nane ($ 800,000) katika mwaka 2014 katika kampeni dhidi ya ujangili nchini. 

Makubaliano hayo yalisainiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Uranium One Inc Bw. Chris Sattler kwa niaba ya Mantra Tanzania (kampuni dada ya Uranium One ambayo inasimamia mradi wa Mto Mkuju, mgodi mkubwa duniani wa uranium katika ukanda wa kusini wa nchi). Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika sambamba na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

“Ujangili wa ndovu umefikia hatua mbaya katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous na kampuni ya Mantra imejipanga kikamilifu kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na tatizo hili,” alisema Bw. Sattler. Aliongeza, “Makubaliano haya yanaturuhusu kushirikiana na Idara ya Wanyamapori, kuandaa na kuutekeleza mpango wa kupiga vita ujangili ili kuwaokoa ndovu waliopo katika hifadhi ya Selous. Napenda kumshukuru Waziri Nyalandu kwa uongozi wake katika suala hili la msingi. Najua wote tunamatumaini kuwa mpango huu utasaidia kuonyesha njia  kwa makampuni binafsi na ya umma kushirikiana katika kuhifadhi wanyamapori Tanzania na Afrika.”

Kwa upande wake, Waziri Nyalandu alisema serikali ya Tanzania, ambayo inaunga mkono Mradi wa Mto Mkuju, itajitahidi kuhakikisha kwamba masuala mengine yaliyosalia kusainiwa yatasainiwa ikiwa ni pamoja na Makubaliano ya Uchimbaji Madini na uendelezaji wa migodi (Mining Development Agreement -MDA-) inatekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni.

 “Jitihada zinazoambatana na hati hii ya kulinda na kutusaidia kupambana na ujangili katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous na pia kupiga hatua zaidi na kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania zitakuwa na maana mara baada ya kusaini MDA. Nategemea kushirikiana na wenzangu toka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Fedha kuhakikisha kuwa tunayafanyia kazi utaratibu zilizobakia ili mradi huo uanze  uzalishaji. “Kwa kusaini makubaliano haya, ninaonyesha njia ya kuwa ni suala linalowezekana kwa seka binafsi na ya umma kufanyakazi kwa pamoja ili kufikia lengo linalokusudiwa,” alisema Nyalandu.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kamati maalum itakayojumuisha wawakilishi wawili kutoka Mantra na wengine wawili kutoka katika Idara ya Wanyamapori itaundwa. Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuandaa, kutekeleza na kuufanyia tathmini mpango huo wa kupiga vita ujangili, na pia kwa ajili ya kuwasiliana na wadau mbali mbali, ikiwa ni pamoja na wawakilishi toka katika ngazi zote za serikali, jamii, makundi ya wawindaji na mashirika yasiyo yakiserikali.

Mkataba huo umejikita zaidi katika kuuendeleza mpango wa vita dhidi ya ujangili, ambao kampuni ya Mantra Tanzania ulishauanza mwaka 2013. Chini ya mpango huu, wahitimu 20 kutoka Chuo cha Mafunzo ya Uaskari wanyamapori cha hifadhi ya Selous wataingizwa katika kitengo cha kampuni ya Mantra cha kupiga vita ujangili. Makubaliano hayo yanaeleza kuwa askari watabaki kuwa wafanyakazi wa hifadhi ya Selous na kurudishwa katika hifadhi baada ya miezi 12 ya kufanya kazi. Wakati kitengo cha kupiga vita ujangili cha Mantra, askari watapatiwa hifadhi karibu na Mradi wa Mto Mkuju na kufanya patroo katika eneo lenye kilometa za mraba 20,000 kuzunguka eneo la mradi.

Mantra itawapatia askari hao mavazi, vifaa na vyombo vya usafiri, pamoja na mafunzo maalum katika mawasiliano, usalama, utafutaji uelekeo na mbinu za kukabiliani na ujangili. Kufanya uchunguzi kwa kutumia ndege maalum inaandaliwa na majaribio ya kutumia magari maalum yenye kamera zitumikazo usiku GPS navigation na video transmitters vimeshakamilishwa. Kufuatana na kufuata taratibu na ruhusa zinazotakiwa, shughuli hizi za ulinzi, zinazounga mkono vita dhidi ya ujangili vitaundwa na kuanza kazi.
Shughuli za Mantra za kupiga vita ujangili pia zitaenda pamoja na mitandao ya ukusanyaji taarifa ya jamii, ambayo itasaidia katika kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa juu ya shughuli za ujangili.