Ushirikiano wa Afrika katika kuhamashjisha kilimo rafiki na
mazingira unalenga zaidi katika kuhakikisha usalama wa chakula katika nchi za
Afrika, juhudi za maendeleo katika kusaidia wakulima wadogo wadogo na katika
suala zima la kilimo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yameelezwa na Bw. Richard Muyungi AMBAE NI MWENYEKITI wa
Ushirikiano wa Afrika katika kuhamasisha kilimo rafiki na mazingira, alipokuwa
akizungumza na wawakilishi kutoka katika nchi za Afrika pamoja na wafadhili
ikiwemo Benki ya Dunia mjini Bonn Ujerumani leo.
Akiiwakilisha Tanzania kama mwenyekiti wa ushirikiano huo, Bwana
Muyungi alisema kuwa, kilimo ndiyo uti
wa mgongo wa nchi za Afrika hivyo kuna haj ya kuboresha mifumo mzima wa kilimo unaozingatia
matumizi endelevu ya rasilimali ya ardhi, kujengea wakulima uwezo kuhusiana na
kilimo chenye tija, na mwisho wa siku kufanikisha suala zima la usalama wa
chakula katika mazingira magumu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Bw. Muyungu aaliongeza kuwa, kilimo katika nchi za Afrika ndio
chanzo kikuu cha kipato na ajira na ni
muhimu sasa kwa nchi za hizo kujikita katikaa kilimo endelevu na matumizi
sahihi ya teknolojia ya kisasa.
Kwa upande mwingine bw. Muyungi alisema kuwa sekta ya kilimo
katika nchi za Afrika ipo katika hatari kubwa kutokana na athari za mabadiliko
ya tabianchi hivyo hatua za haraka zainatakiwwa kuchukuliwa katika kuhakikisha kunakuwepo
na usalama wa chakula,
Lengo kubwa la Ushirikiano huu ni kuhakikisha kuwa nchi za
Afrika zinaongeza tija katika kilimo, zinazingatia hifadhi ya mazingira na kujengewa
uwezo kuhusu kilimo rafiki na mazingira kitakachosaidia kuhimili athari za
mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza uzalishaji wa gesijoto kupitia sekta ya
kilimo..