NEWS ALERT: AKAMATWA NA MENO YA TEMBO VIPANDE 8 VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 45

Na  Walter  Mguluchuma Mpanda Katavi Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Rashid  Ramadhani (Bonge)  (31) Mkazi wa Mtaa wa  Nsemlwa  ... thumbnail 1 summary
Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Rashid  Ramadhani (Bonge)  (31) Mkazi wa Mtaa wa  Nsemlwa  Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi  anashikiliwa na jeshi la polisWilaya Mpanda  Mkoani  wa Katavi kwa tuhuma   za   kukamatwa na meno ya Tembo  vipande  nane vyenye uzito wa kilogramu  14  yenye thamani ya shilingi milioni  45

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi  mwandamizi Dhahiri Kidavashari  mtuhumiwa  huyo alikamatwa  hapo mei  20  mwaka huu  majira ya saa mbili na nusu usiku  katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa  Rex  iliyoko  katika  mtaa wa Majengo A Mjini   Mpanda 

Alisema  siku hiyo ya tukio mtuhumiwa  akiwa na mwenzake mmoja  ambae  bado hajafamika  walifika kwenye nyumba ya kulala wa  geni hiyo ambayo alikuwa amefikia  Rashid  huku wakiwa na  mkokoteni  waliingia ndani ya  Guest hiyo na  na kutowa  vipande hivyo vya meno ya tembo  ambavyo  vilikuwa vimeviringishwa kwenye  mfuko wa sandarusi   na kuvipakia kwenye mkomkoteni huo

Alifafanua kuwa  baada ya kuwa wamepakia   meno hayo ya Tembo  kwenye mkokoni huo raia  wema  ambao walikuwa kwenye eneo  waliweza kubaini kilichokuwa  kinaendelea  na  ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la Polisi huhusiana natukio hilo 

Kamanda Kidavashari  alieleza  baada ya jeshi la polisi  kutapa taarifa hizo kutoka kwa Raia wema  waliandaa mtengo  kwa kushirikiana  na Askari wa Wanyama piri wa Hifadhi  ya mbuga ya Katavi  katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mpanda 

Alisema askari hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Rashid  akiwa na meno hayo ya Tembo  wakati akiwa  anasukuma mkokoteni huo muda mfupi tuu baada ya kuondoka kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni   akiwa analekea kwenye Stendi ya  mabasi ya Mpanda  na huku mwenzake aliyekuwa nae awali  akiwa ameisha tokomea kusiko julikana

Alieleza baada ya kufanya upekuzi kwenye mzigo huo ndipo Askari polisi na  askari wa Tanapa  walipoweza kukuta meno ya Tembo vipande nane vyenye uzito wa kiligramu 14 vya thamani ya  Tshilingi  milioni 45  vikiwa  vimeifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi

Kamanda Kidavashari  alisema  upelelezi wa   tukio hilo  unaendelea  na juhudi za kumsaka  mtuhumiwa  aliyekimbia   pamoja nakuweza kubaini  kubaini vyanzao  na mtandao  wa  watu  wanahusika  katika biashara  hii haramu  ya meno ya Tembo

Mtuhumiwa  Rashid Ramadhani  anatarajiwa  kufikishwa  mahakamani wakati wowote  kuhusiana na shitaka  linalomkabili  baada ya  uchunguzi   utakapo  kuwa umekamilika
Mwisho