Nimekuwa
nikichunguza sana katika Sherehe mbalimbali hasa hizi za Harusi, ambapo
huanza kwa kuagwa kwa Binti na Baadae kuwa na Harusi yenyewe, kwa kweli
Vijana wanajitahidi sana kutokelezea ki Afrika zaidi siku hizi za
karibuni kwa kuvaa nguo ambazo asili yake ni ya hapa hapa Afrika, lakini
Pia Mabinti hujitahidi sana kuvaa nguo za Kiafrika hasa wakati wa
Kitchen Party pale wanapo wafunda .
Lakini
tatizo linakuja sasa wakati wa Harusi kila mtu anataka kuvaa nguo kama
wazungu na kusahau kwamba kuna hizi za Kiafrika ambazo pengine wangevaa
zaidi wangependeza zaidi kwa sababu zinaelezea u Afrika kabisa na
kuvutia zaidi.
Zifuatazo ni Picha ambazo zinaonesha Dhahili jinsi ambavyo utapendeza katika Harusi yeko endapo utavalia ki Afrika zaidi
Tazama
kwa umakini Bibi na Bwana walivyo pendeza Wamevalia Nguo za kawaida
kabisa lakini zenye kiwango cha juu, ukiwatazama hawa wameongezeka uzuri
zaidi ni kutokana na haya mavazi yao
Huu ni ubunifu wa Hali ya Juu tazama Nguo ya Kiafrika ikiwa imefanana kabisa na ua ambalo amebeba
Wewe
unaesoma hii sasa hivi hii kitu hebu tazama kwanza .. na haujaoa wala
kuolewa unangoja nini sasa? hawa jamaa wamependeza sana na mavazi yao
ambayo yamebuniwa ki Afrika zaidi
Sio lazima mpaka mvae Shela...
Hii
harusi moja kwa moja itakuwa imefungiwa kijijini lakini pia hawa watu
wanaonekana ni wa mjini ingawa hapa wamevalia mavazi yao ya asili ya
Kiafrika katika Harusi yao.
Amependeza hajapendeza?
Ukiangalia
kwa umakini vazi hili la huyu binti lina mambo mengi sana, kwanza
ukitazama hapa lina manyoya ya ndege halafu kisha inapendeza sana hapa
akikolezea na hii nyeupe ... hebu rudini jamani ambao hamjaoa wala
kuolewa hii ni nafasi yenu
Binti wa Kizungu akiwa ki Afrika zaidi
Sitii neno
Hebu watazame hawa kuanzia juu mpaka chini nazani na wewe utapata kitu hapa...
Mwisho Vijana wenzangu ambao bado hamna ndoa hebu ikifika mvae japo kama hawa itakuwa poa sana
Imeandaliwa na Fredy Njeje Blog