Chanzo: Stratton Hatfield
Katika
kujiokoa kwenye hatari yeyote ile si tu watu ambao wanaweza kupata wazo
la ajabu la kutenda ilimradi tu kuepukana na mauti, fisi mmoja
aliyekuwa katika lishe yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kulazimika kujificha kwenye tumbo la mzogo wa tembo ili kumkwepa simba
dume aliyemvamia ghafla.
Fisi
huyo aliyaona mauti yaleeeeee, lakini aliona ni heri kukaa ndani ya
tumbo la tembo kulikoni kuliwa na simba. picha zifuatazo zinaonyesha
namna fisi huyo alivyojificha na baadae kufanikiwa kukimbia baada ya
kupata upenyo.
Tukio hilo halijatokea mbali bali ni kule Masai Mara, pata uhondo huo..