SHUHUDIA SIMBA KUTOKA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI ALIYEISHI NA WAYA SHINGONI KWA MUDA WA MIAKA MITATU, APONA BAADA YA MATIBABU.

Huyu ni Simba Mdogo ambaye tokea akiwa mdogo alikuwa amevalishwa waya shingoni na kukuwa nayo mpaka anafikisha Miaka Mitatu hali ambayo... thumbnail 1 summary
Huyu ni Simba Mdogo ambaye tokea akiwa mdogo alikuwa amevalishwa waya shingoni na kukuwa nayo mpaka anafikisha Miaka Mitatu hali ambayo ilipelekea shingo yake kukuwa na kuendelea kuumizwa na waya huo mpaka alipokuja kuokolewa kwa maana ulikuwa unambana na kuendelea kumchana.

Simba huyo kwa mara ya kwanza alifanyiwa mawindo ilikuwa ni mwaka 2009 katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi lakini juhudi hizo hazikufanikiwa na ilikuwa ni zaidi ya Mara saba lilifanyika zoezi la kumkamata bila matumaini yoyote.


Baada ya miaka mitatu kupita Shingo ya Simba huyo ilizidi kuharibika kwa msuguano wa ule waya na kusababisha akose nguvu za kuwinda na wadudu walianza kumtembelea katika kidonda jambo ambalo lingeweza kumsababishia matatizo zaidi na hata magonjwa.
Juhudi za kumfuatilia simba huyo ziliendelea na baadaye Simba huyo aliyeteseka sana alikamatwa na kutolewa waya shingoni kisha kufanyiwa Matibabu.


Kutokana na maelezo ya Mlezi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Ndugu William Mwakilema alisema kwamba wakati Simba huyo anakamatwa alikuwa bado ana hali dhoofu na alikuwa hana uwezo hata wa kuwinda tena.

 Picha mbalimbali zikimuonesha Simba huyo na jinsi alivyo okolewa.


 
Hivi ndivyo Shingo ya Simba huyo ilivyo haribika baada ya kukaa na waya wa umeme shingoni kwa muda wa miaka mitatu



 Baadhi ya Askari wa wanyama pori wakiwa wanamtoa simba huyo kamba shingoni
Mlezi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi bwana William Mwakilema akionesha waya ambazo alifungwa simba huyo akiwa mdogo na kukuwa nazo kwa Miaka Mitatu

 Picha hiii ikimuonesha Simba huyo aliyekuwa na waya shingoni kwa muda wa Miaka Mitatu sasa amepona.