Ukarabati Uwanja wa Ndege waila bajeti Zanzibar

Wajumbe wa Baraza la Wakilishi wamepitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa fedh... thumbnail 1 summary
Wajumbe wa Baraza la Wakilishi wamepitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2014/15 huku ujenzi wa Uwanja wa Ndege ukichukua kiasi kikubwa cha bajeti hiyo.
Hayo yalithibitika wakati wajumbe wote waliponyanyua mikono kuashiria kukubaliana na yote yaliyomo katika bajeti hiyo ya Serikali.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee alishukuru wajumbe hao akisema atahakikisha upungufu wote uliojitokeza unafanyiwa kazi.
“Haya ni matumizi yetu kwa maana hiyo tushirikiane ili kutekeleza kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.
Kutokana na kupita kwa bajeti hiyo, ni dhahiri sasa Zanzibar itaweza kutumia kiasi cha Sh707.8 bilioni kwa mwaka wa fedha 2014/15 katika kuendesha shughuli zake.