UMOJA WA WAKE WA VIONGOZI 'NEW MELLINIUM WOMEN GROUP' WATEMBELEA KAMBI YA MAISHA PLUS NA MAMA SHUJAA WA CHAKULA BAGAMOYO

  Mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group Mama Tunu Pinda akiwongoza wakina mama wenzake kuelekea katika kambi ya... thumbnail 1 summary
 Mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group Mama Tunu Pinda akiwongoza wakina mama wenzake kuelekea katika kambi ya Maisha Plus aliye nyuma yake ni Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali. Wakina mama hao walifika katika kambi hiyo ili kujionea shughul zinazo fanywa na washiriki katika maisha Plus iliyopo Bagamoyo Pwani
 Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali akiwa na Mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group  Mama Tunu Pinda pamoja na Katibu wa chama hicho cha wake wa viongozi Mama Pamela Mathayo wakiangalia shamba la mfano ambalo washiriki wa maisha Plus wanaliandaa.
 Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali akiwasha jiko la gesi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa gesi inayo tokana na kenyesi cha ng’ombe ambayo imetengenezwa na washiriki wa maisha plus kulia kwake ni mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group   Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda   wakiwa na wake viongozi  wakishuhudia uzinduzi huo ambao umefanyika katika kambi ya Maisha Plus iliyopo wilayani Bagamoyo Pwani Picha na Chris Mfinanga.
Wanachama wa cha wake wa Viongozi New Mellinium Women Group wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maisha Plus wa hapa nchini na nnje ya nchi pamoja nawaandaji. (Picha zote na Chris Mfinanga)



Kijiji cha Maisha Plus chapata ugeni mkubwa waliotembelea kjijini hapo kujionea mambo mbalimbali yanayofanyika. Ugeni huo ulifika kijijini hapo baada ya kumaliza shughulisha ya kusafisha kisima cha kijiji ili kuwa na uhakika wa maji safi na salama na wengine walikuwa na katika pilika pilika za mapishi. 

Wanakijiji waliwalaki wageni hao kwa shangwe ambao ni wake wa viongozi wa nchi ngazi za juu akiwemo mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda, Makamu wa Rais mama Aisha Bilal, mama Gervina Lukuvi, Mama Sophia Kawawa, Mama Mgufuli na wengineo.

Ugeni huu ni mkubwa kwa wanakijiji cha Maisha Plus kwani hawakutegemea kupata ugeni huo hivyo walifurahi na kupata faraja zaidi pamoja na kuona kuwa mchango wao unatambuliwa kitaifa na kuthaminiwa na viongozi nchini. 

Ugeni huu ulipata fursa ya kutembelea kila kaya kijijiini hapo na kujionea kazi za ubunifu walizofanya kwa kipindi kifupi cha siku tano ambapo miradi mbalimbali ya kuvutia iliibuliwa na kuonyesha ujuzi na ubunifu wa hali ya juu waliokuwa nao wanakijiji hao unaoendana na mazingira yanayowazungka. 

Miradi hiyo ni pamoja na utengenezaji wa sabuni ya aji na kipande, batiki, bustani za kuhama, aina mbalimbali za majiko yanayotumia kuni chache, kikapu cha ajabu kinachotunza chakula kisipoe na kuivisha chakula pia, ufugaji bora na wa kisasa wa kuku na nyuki, jiko la gesi na mengine mengi.

Wakati wa kutembelea kaya za kijijini hapo alikaribishwa katika familia ya Shida Keneth Mganga na kupata chakula cha mchana na familia hiyo ingawa hakupendezwa na jina la hilo na kumpatia jina la TUnu. Vile vile alikabidhi kiasi cha shilingi 70,000/= kwa Malkia wa kijiji Pendo Mussa kama mchango wao kwa wanakijiiji hao.

Wakati alipokuwa akiongea na wanakijiji cha Maisha Plus mama Aisha Bilal alisifu kazi hizo kwani zilitengeneza kwa ubunifu mkubwa na kuwasisitiza wanakijiji waendelee kufanya hivyo kujiletea maendeleo katika jamii. Naye Mama Tunu Pinda aliwaeleza wanakijiji kuwa waendelee kuwa mabalozi wazuri na kuwa mfano wa kuigwa na chachu katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii. 

Aliongezea na kusema kuwa kuna haja ya Maisha Plus kuwa na eneo kila mkoa na kuwekeza katika miradi endelevu itakayowanufaisha washiriki na jamii kwa ujumla. Sambamba na hayo mama Tunu Pinda, Aisha Bilal na Germin Lukuvi walikabidhi mawadawa 30 yaliyotengenezwa na wanakijiji hao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ndugu SamwSalianga.