WAKE WA VIONGOZI WA NCHI AKIWEMO MAMA TUNU PINDA,MAMA AISHA BILAL,MAMA GERVINA LUKUVI, MAMA MAGUFULI NA WENGINE WATEMBELEA KIJIJI CHA MAISHA PLUS.

Kijiji cha Maisha Plus chapata ugeni mkubwa waliotembelea kjijini hapo kujionea mambo mbalimbali yanayofanyika. Ugeni huo ulijumuisha wake ... thumbnail 1 summary

Kijiji cha Maisha Plus chapata ugeni mkubwa waliotembelea kjijini hapo kujionea mambo mbalimbali yanayofanyika. Ugeni huo ulijumuisha wake wa viongozi wa nchi ngazi za juu akiwemo mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda, Makamu wa Rais mama Aisha Bilal, mama Gervina Lukuvi, Mama Magufuli na wengineo.


Wanakijiji ambao wakati wageni hao wanafika walikuwa katika pilika pilika za mapishi na wengine walikuwa wamemaliza kusafisha kisima waliwalaki kwa shangwe kwani hawakutegemea kupata ugeni huo hivyo walifurahi na kupata faraja zaidi pamoja na kuona kuwa mchango wao unatambuliwa kitaifa na kuthaminiwa na viongozi nchini.

Ugeni huu ulipata fursa ya kutembelea kila kaya kijijiini hapo na kujionea kazi za ubunifu walizofanya kwa kipindi kifupi cha siku tano ambapo miradi mbalimbali ya kuvutia iliibuliwa na kuonyesha ujuzi na ubunifu wa hali ya juu waliokuwa nao wanakijiji hao unaoendana na mazingira yanayowazungka.
 Miradi hiyo ni pamoja na utengenezaji wa sabuni ya maji na kipande, batiki, bustani za kuhama, aina mbalimbali za majiko yanayotumia kuni chache, kikapu cha ajabu kinachotunza chakula kisipoe na kuivisha chakula pia, ufugaji bora na wa kisasa wa kuku na nyuki, jiko la gesi na mengine mengi.
Wakati wa kutembelea kaya za kijijini hapo mama Tunu Pinda alikaribishwa katika familia ya Shida Keneth Mganga na kupata chakula cha mchana na familia hiyo ingawa hakupendezwa na jina la Shida hivyo kumpatia jina la Tunu.
Vile vile alikabidhi kiasi cha shilingi 700,000/= kwa Malkia wa kijiji Pendo Mussa kama mchango wao kwa wanakijiiji hao.

Wakati alipokuwa akiongea na wanakijiji cha Maisha Plus mama Aisha Bilal alisifu kazi hizo kwani zilitengenezwa kwa ubunifu mkubwa na kuwasisitiza wanakijiji waendelee kufanya hivyo kujiletea maendeleo katika jamii.
Naye Mama Tunu Pinda aliwaeleza wanakijiji kuwa waendelee kuwa mabalozi wazuri na kuwa mfano wa kuigwa na chachu katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii.

Aliongezea na kusema kuwa kuna haja ya Maisha Plus kuwa na eneo kila mkoa na kuwekeza katika miradi endelevu itakayowanufaisha washiriki na jamii kwa ujumla. Sambamba na hayo mama Tunu Pinda, Aisha Bilal na Germin Lukuvi walikabidhi madawati 30 yaliyotengenezwa na wanakijiji hao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ndugu Samwel Salianga.Wakati alipokuwa akiongea na wanakijiji cha Maisha Plus mama Aisha Bilal alisifu kazi hizo kwani zilitengeneza kwa ubunifu mkubwa na kuwasisitiza wanakijiji waendelee kufanya hivyo kujiletea maendeleo katika jamii. Naye Mama Tunu Pinda aliwaeleza wanakijiji kuwa waendelee kuwa mabalozi wazuri na kuwa mfano wa kuigwa na chachu katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii. Aliongezea na kusema kuwa kuna haja ya Maisha Plus kuwa na eneo kila mkoa na kuwekeza katika miradi endelevu itakayowanufaisha washiriki na jamii kwa ujumla. Sambamba na hayo mama Tunu Pinda, Aisha Bilal na Germin Lukuvi walikabidhi mawadawa 30 yaliyotengenezwa na wanakijiji hao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ndugu SamwSalianga.