WAZIRI NYALANDU AIPONGEZA KLM KWA KUKUZA UTALII NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akimsikiliza kwa makini Meneja Mkuu wa KLM kwa upande wa Africa Mashariki Bw. Dr... thumbnail 1 summary

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akimsikiliza kwa makini Meneja Mkuu wa KLM kwa upande wa Africa Mashariki Bw. Dries Klein wakati hafla ya maadhimisho ya kutimiza miaka 45 ya Shirika la KLM kufanya kazi nchini yaliyofanyika jana jijijni Dar es Salaam.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amelipongeza shirika la ndege la KLM kwa mchango wao mkubwa wa kusaidia Tanzania katika kukuza utalii tangu kuanzishwa kwake mwaka 1969.
Aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya Shirika la ndege la KLM yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Nyalandu alisema anathamini sana mchango wa shirika la KLM kwa kuwa wavumilivu na wastahimilivu licha ya kuwa nchi imekuwa ikikumbwa na mdororo wa kiuchumi lakini KLM wamekuwa wakiendelea kutoa huduma zao bila kujali kuwa wanapata faida kwa kiasi gani ikiwa na tofauti na mashirika mengine ya ndege ambayo yamekuwa yakisitisha kutoa huduma pindi nchi inapokuwa kwenye hali ngumu ya kiuchumi.
‘’KLM ni shirika la ndege la pekeee nchini Tanzania, kwani lina historia ndefu kwa taifa letu katika kuleta maendeleo na kutoa huduma bora kwa Watalii wanaokuja nchini, Hivyo hatuwezi kujivunia kukua kwa sekta ya Utalii nchini pasipo kuwataja KLM’’ Mhe. Nyalandu alisisitiza
Mhe. Nyalandu amelitaja Shirika la KLM kuwa ni kichocheo cha maendeleo hapa nchini kwani tangu kuanzishwa kwakemwaka 1969 limeitangaza Tanzania katika Nyanja za kimataifa katika masuala ya Utalii na hivyo Tanzania imekuwa ikifahamika kuwa ni ardhi ya Mlima Kilimanjaro, ardhi ya Zanzibar na kwa sasa Tanzania imeanza kufahamika kuwa ni ardhi ya Serengeti kwa kuwa na vivutio vya vingi ambavyo havipatikani sehemu yoyote duniani.
Meneja wa KLM kwa upande kwa Afrika Mashariki Bw. Dries Klein amempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Nyalandu kwa kuthamini na kutambua mchango wao wa kukuza Utalii nchini tangu nchi ilipokuwa ina miaka tisa tu baada ya kupata uhuru wake .’’ Najisikia fahari pamoja na Wafanyakazi wangu wote wa KLM kwa kutoa huduma bora na zenye kiwango cha kimataifa kwa wenyeji pamoja na wageni mbalimbali ambao huja kuitembelea Tanzania.
Bw . Dries Klein aliongeza kuwa shirika la KLM linajivunia kufanya kazi Tanzania kwa kuwa linathaminiwa na serikali ya Tanzania kwa kupitia Mamlaka ya anga (ATCL) nchini hivyo wamejikuta wakitoa huduma pasipo matatizo yoyote , ‘’Tunamwahidi Mhe . Nyalandu tutaendelea kufanya kazi nchini na kutangaza utalii kama tulivyoweza kufanya mwaka 2013 kwa kuwaleta watalii million moja nchini kuja kuona vivutio mbalimbali.
Mhe. Nyalandu aliongeza kuwa licha Utalii kukua kwa kasi nchini lakini hata hivyo kama vita dhidi ya Ujangili havitapiganwa kwa ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya nchi wenda Shirika la KLM likakosa wateja kwa siku za mbeleni ambapo huja nchini kwa ajili kuona vivutio mbalimbali.