Bw.
Anic Kashasha, Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali
Tanzania Creative Industries Network (TACIN) ya Dar es Salaam, nilikuwa
ninahutubia mkutano wa waandishi wahabari kwenye ukumbi wa Safari
Lounge, mjini Mtwara, juu ya kuanzisha Mtwara Festival, utakaofanyika
tarehe 16 - 17 Agosti, 2014 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona,Mtwara.
Mtwara
Festival imeandaliwa kwa kushirikiana na washirika wakuu na wadhamini
wa TACIN, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Huu ni
mkakati endelevu wa mawasiliano ili kuwahasisha wananchi wa mikoa ya
Mtwara na Lindi, kuzitambua, kujiandaa na kuzichangamkia fursa
zinazotokana na uiwekezaji mkubwa unaendelea katika mikoa hiyo.
Mtwara
Festival itakuwa ni tukio la kila mwaka kwa malengo ya kuitangaza mikoa
ya Mtwara na Lindi kama mikoa yenye vivutio vingi vya utalii wa
utamaduni ikiwa ni pamoja na uchongaji wa vinyago vya na ngoma
mbalimbali zenye mvuto Mkubwa. Bodi ya Utalii (TTB) ni Wadau katka
mpango huu na watautangaza kupitia njia zake zote yaani mtandaoni, DVD,
na majarida yatumikayo kuitangaza Tanzania kwenye Masoko mbalimbali
duniani kote. Aidha, TTB wataiweka Mtwara Festival kwenye kalenda ya
matukio ya ki- utalii ya Tanzania.
Wenyeji
wa Mtwara Featival ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mtwara (V). Chama cha Wafanyaniashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA)
tawi la Mtwara nao ni washirika wa mpango huu.