Maliasili Mpanda wakusanya zaidi ya shilingi milioni 260

Na  Walter  Mguluchuma  Mpanda  Katavi Halmashauri ya  Wilaya  ya Mpanda  imekusanya zaidi ya shilingi milioni 260  zilizotokana  na... thumbnail 1 summary
Na  Walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
Halmashauri ya  Wilaya  ya Mpanda  imekusanya zaidi ya shilingi milioni 260  zilizotokana  na mapato ya  ndani  zilizokusanywa  na Idara  ya Ardhi  na Maliasili  katika kipindi cha mwaka mmoja  kuanzia  julai  2013  hadi june 2014
Haya yalielezwa  hapo juzi  na Kaimu  Afisa   Ardhi na  Maliasili  na  Mazingira    wa Halmashauri ya   Wilaya  ya Mpanda  Josephina Rupia  wakati akitoa  taarifa ya utekelezaji  wa  shughuli  za idarahiyo   kwa kipindi  cha mwaka  2013 na 2014 kwenye  mkutano  mkuu wa  mwaka  wa Baraza  la madiwani  wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mpandauliofanyika kwenye ukumbi wa maji  mjini  hapa
Alisema Idara hiyo  imewaza kukusanya jumla ya  shilingi  265,290,050 kwa kipindi cha julai 2013  hadi june mwaka huu zilizotokana  na  mapato ya  ndani
Rupia alifafanua  shilingi  milioni 260,780, 000 zilitokana  na  ushuru  wa leseni za mbao Tsh  210,750 ushuru wa Magobole ,Tsh  296,500 ushuru wa asali na kuingia polini  Tsh914,000 ada ya fomu za viwanja  na Tsh  3,868,800 ushuru wa  uwindaji wa kienyeji
Alisema  katika  kipindi  hicho  cha mwaka mmoja  idara hiyo  imeweza kufanya  doria mbili kubwa  na kufanikiwa  kukamata  mbao  na magongo yalivumwa bila kibali  pamoja na magunia  369 ya mkaa na wanasishililia baiskeli  tisa  ambazo wavunaji haramu wa maliasili walikimbia na kuziacha
 pia wamewaza  kukamata Ng’ombe  280  ambazo   zilikuwa zimeingizwa kwenye msitu wa hifadhi  wa  Nkaba  na wamiliki watatu  wa mifugo hiyo  wamefunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani
Josephina  Rupia alilieleza  baraza hilo na madiwani walikuwa wakiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yassin Kibiriti  idara hiyo imeweza  kufanya operesheni  ya  kuondoa  makazi holela  na watu 361 wameondolewa kwa nguvu  na kati yao 15  wamefikishwa mahakamani
Alifafanua  idara hiyo   imefanya  mpango  bora wa matumizi ya adhi  katika  kijiji  cha  Lwega  Tarafa ya Mwese  na wanatarajia  kuendelea katika  vijiji  vya Katuma na  Kapanga
Alisema  wametatua baadhi ya migogoro ya mipaka kwenye baadhi ya vijiji kwa  kuzikutanisha  pande zote mbili  zilizokuwa  na migogoro ya kugombea mipaka kwenye vijiji  vyao