MWAKYEMBE ATIMUA WAFANYAKAZI 11 UWANJA WA NDEGE

             Waziri wa uchukuzi nchini Tanzania mh  HARSON  MWAKYEMBE amewafuza kazi katika uwanja wa ndege muda huu watumishi takribani ... thumbnail 1 summary
             Waziri wa uchukuzi nchini Tanzania mh  HARSON  MWAKYEMBE amewafuza kazi katika uwanja wa ndege muda huu watumishi takribani 11 kutoka katika wizara za kilimo,afya,pamoja na wizara ya mifugo na uvuvi,kwa kushindwa kufwata taratibu za kazi katika uwanja wa ndege wa JK NYERERE jijini Dar es salaam.
     
         Akizungumza na Wanahabari muda huu ofisini kwake waziri MWAKYEMBE Amesema kuwa watumishi  wamekiuka sheria za kazi kutokana na kuendekeza vitendo kama vya rushwa,ubaguzi uwanjani hapo jambo ambalo Amesema kuwa hawezi kufumbia macho vitendo kama hivyo viendelee katika uwanja huo
      
            “Tunahangaika sana kupambana na madawa ya kulevya katika uwanja wetu wa jk nyerere,sasa wanajitokeza watu ambao sio waaminifu wanatuharibia sifa ya uwanja wetu kwa sababu zao,kiukweli hatuwezi kuvumilia tabia hizo na kuanzia sasa saa sita mchana sitaki kuwaona pale na nimeagiza waondolewe na polisi warudishwe maofisini kwao”alisema MWAKYEMBE.
      
         Hatua hiyo imekuja baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko kutoka nchi za uarabuni,india na china kufanyiwa upekuzi tofauti na wengine na kuchukuliwa vyakula vyao na bidhaa mbalimbali kinyume na sheria ambapo bidhaa hizo zimekuwa hazirudishwi kwa wenyewe.
Waziri MWAKYEMBE amewataja wahusika hao kuwa ni -
                                  
                             Wizara ya kilimo
1-TEDDY MWASENGE
2-ESTER KILONZO
3-REHEMA MRUTU
4-MARY KADOKAYOSI
5-KISAMO SAMJI
6-ANNETH KILIANGA
                               
                                     Wizara ya afya
1-AGNESS SHIRIMA
2-HAMIS BORA
3-VALERI CHUWA
4-ELINGERA MGHASE
5-REMEDIUS KAKULU
                              
                                 Wizara ya mifugo na uvuvi
1-ESHI SAMSON NDOSI
2-ANNE SETEBE

            Aidha waziri MWAKYEMBE ametoa onyo kali sana kwa wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JK NYERERE watakaoingia kwa sasa kutojihusisha na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria ikiwemo rushwa kwani wizara yake haitawavumilia hata kidogo