Picha: Barabara iliyojengwa juu zaidi Tanzania

Kibao kinachoeleza vipimo namna barabara hii iliyvo.  muonekano wa kibao ukiwa usawa wa chini kidogo kutoka usawa wa ... thumbnail 1 summary
Kibao kinachoeleza vipimo namna barabara hii iliyvo. 

muonekano wa kibao ukiwa usawa wa chini kidogo kutoka usawa wa barabara.

Upande wa kushoto ni barabara maeneo ya kawetele lakini kulia ni muonekano wa muinuko ilikopita barabara.

ukiwa juu utaweza kuona muonekano wa bonde la ufa kama lionekanavyo katika picha hii.

Barabara hii inaanzia standi ya mwanjelwa inapitia isanga kuelekea Chunya,  ambapo barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani kama Singida, Dodoma na Tabora. uwapo safarini alama pekee ya kukufanya utambue umefika maeneo ya kawetele ni hali ya hewa safi na mwana ambapo eneo hili limewekwa vipimo vya hali ya hewa(Airpoint).

Mahali hapa barabara ipo juu kuliko barabara zote nchini Tanzania, Eneo hili lipo barabara ya Chunya nje kidogo ya jiji la Mbeya, uwapo juu kawetele Utaweza kutizama mandhari ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, linalopitia maeneo ya mji wa mbeya, utaweza kuona Bonde la Usangu na maeneo kama Inyala, Chimala, Igurusi, Itamba, Msesule na kadhalika. pia Utafurahia sana kuiona reli ya Tanzania Zambia Railway (TAZARA) inavyolizunguka eneo hilo.

Karibu Tanzania, Karibu Mbeya.
 
Chanzo: Mbeya home of tourism