Sitowachekea wachafuzi wa Mazingira - Dkt. Mahenge

 Na Rashda Swedi- VPO Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratib... thumbnail 1 summary
 Na Rashda Swedi- VPO
Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratibu na sheria za utunzaji wa Mazingira, ameseme jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipofanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta (Murza Oil Mills Limited) kilichopo Vingunguti. 
Dkt Mahenge alisema hayo baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo wa maji taka kwa lengo la kulinda mazingira kwa sababu wasipofanya hivyo Serikali itachukua hatua ya kukifunga kiwanda hicho. 
Wakati huo huo, mwanasheria wa NEMC Bw.Manchale Heche amesema kuwa, kutokana na ziara waliyoifanya pamoja na Mh. Waziri wamegundua mengi na hawatafumbia macho suala la viwanda vinavyotumia magogo, kuni na wale wasiokuwa na mfumo mzuri wa majitaka endapo hawatafuata masharti waliyokubaliana nayo viwanda hivyo vitafungiwa. 
Waziri alitembelea pia bwawa la maji taka lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam na kugundua kuwa kuna uharibifu mkubwa wa Mazigira, kutokana na maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali karibu na eneo hilo kutiririsha maji yao kwenye mabwawa hayo.
Kutokana na hilo amewataka Manispaa kushirikiana na NEMC kuvijua viwanda vinavyopitisha maji machafu moja kwa moja bila kufuata utaratibu uliowekwa.
 "Ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira na sio wajibu wa Ofisi ya makamu wa Rais tu kwani Mazingira ni yetu sote na ni muhimu kuyalinda" Mh. Mahenge alisema.Alisisitiza kuwa, huo hautakuwa mwisho wa ukaguzi wa viwanda utaratibu wa kukagua viwanda utaendelea kuangalia Mazingira rafiki kwa wananchi.
 Meneja wa kiwanda cha Murza Oil Mills Limited Bw. Dinesh Kana (wa tatu kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kushoto) kuhusu mfumo wa maji taka ambao wanautumia katika kiwanda hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala bw. Abdon Mapunda (wa pili kushoto) alipotembelea bwawa la maji taka la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
 Maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali vilivyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ambayo hutiririsha maji yake katika mto wa msimbazi, maji ambayo yanahatarisha afya ya binadamu
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Bw. Richard Matari ambaye ni msimamizi wa dampo la Kinyamwezi lililopo Pugu jijini Dar es Salaam, baada ya waziri kuwasili katika dampo hilo na kutaka kujua utendaji wa kazi zao katika kulinda Mazingira.
Sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi lilopo jijini Dar es Salaam.