Tembo, faru hatarini kutoweka

  VITENDO vya ujangili vinavyoendelea kushamiri nchini, vimechangia taifa kukumbwa na hatari ya kutoweka kwa wanyamapori wakiwemo tembo... thumbnail 1 summary
Tembo, faru hatarini kutoweka 
VITENDO vya ujangili vinavyoendelea kushamiri nchini, vimechangia taifa kukumbwa na hatari ya kutoweka kwa wanyamapori wakiwemo tembo na faru.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa na Profesa Davis Mwamfupe wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya kuwajengea uelewa wabunge katika kulinda wanyamapori, iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge cha Kuhifadhi na Kulinda Wanyamapori.

Profesa Mwamfupe alisema hivi sasa wanyama hao ambao walikuwa wengi katika mbuga na hifadhi mbalimbali nchini, wamepungua kwa kiasi kikubwa.


Alisema hakuna takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa wanyama hao, bali kupungua kutokana na vitendo vya ujangili.


Alieleza kuwa hali hiyo inatokana na uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na faida za wanyamapori.
“Hali hii ndiyo iliyotupa mwamko wa kutoa elimu kuhusiana na hifadhi za wanyamapori na thamani ya wanyama hao, lakini pia hali halisi inayoendelea hivi sasa kuhusiana na wanyamapori,” alisema.