KIBOKO AVAMIA KIJIJI WANANCHI WASHINDA JUU YA MITI KUTWA NZIMA

Na   Walter   Mguluchuma Mpanda Katavi Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya Mashimboni   wilaya ya Mlele Mkoa wa... thumbnail 1 summary
Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya Mashimboni  wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelazimika kushinda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko  aliyevamia kijiji hicho  na kuhatarisha uhai wa Wanachi
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Mashimboni  Raphael  Kalinga  tukio hilo  lilitokea hapo Agos 18 majira ya saa  moja na nusu asubuhi
Akielezea tukio hilo alisema  Kiboko huyo baada  ya kuvamia kijiji hicho  alielekea  kwenye nyumba ya mkazi  mmoja  aitwaye Joseph  Kashamakula  ambae  alinusurika  kushambuliwa na Biboko huyo wakati alipokuwa  akitokea chooni kujisaidia
 Diwani  Kalinga alisema  ndipo Kiboko huyo ambae  alionekana kuwa na hasira alipoanza  kukanyaga  kanyanga na vuvivunja vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa  nje ya nyumba yake na kuviharibu kabisa  hari ambayo ilimfanya  wananchi huyo apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani
Majirani walifika kwenye eneo hilo  hata hivyo walilazimika  kutimua mbio  baada ya kiboko huyo  kuanza  kuwafuata  hari ambayo ilipelekea  kukimbia na kisha kupanda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na mnyama huyo ambae aliendelea kuvunja vyombo kwenye nyumba mbalimbali
 Alisema  Kiboko huyo aliendelea kuzunguka kwenye eneo la kijiji hicho na  taarifa za  zilifika kwenye Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya  Nsimbo  ambao  walituma Akari wao wa wanyama pori kwenda huko
Baada ya  Askari wa Maliasli kufika kijijini hapo  walianza msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi  ambapo walifanikiwa kumwona na kisha  walimuuwa kwa kumpiga Risasi  tumboni na kichwani
Diwani   Kalinga  alieleza  baada ya Kiboko kuuwa  wananchi  licha ya hapo awali kumkimbia kiboko huyo  walianza  kugombea  nyama  ya  mnyama huyo  kwa kuchukua  kitoweo cha mboga na  baada ya nusu saa wakawa wamemmaliza