Video nyingine inayoonyesha uwindaji haramu unavyotekelezwa mchana kweupe Tanzania

Hivi karibuni Peter Msigwa aliweka hadharani video inayoonyesha wahusika wa Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Limited, wakitenda uh... thumbnail 1 summary
Hivi karibuni Peter Msigwa aliweka hadharani video inayoonyesha wahusika wa Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Limited, wakitenda uhalifu wa wazi dhidi ya wanyama, wakikiuka sheria za Tanzania na kimataifa katika uwindaji.

Juzi Ijumaa tarehe 12 Agosti 2014, Motherboard wametoa video nyingine ikionyesha uharamia dhidi ya wayanma uliokuwa unafanywa na Green Miles Safaris Limited.

Inadaiwa kuwa video ni sehemu ya video ndefu ya karibu masaa mawili inayoonyesha wakiwaua wanyama wakiwa kwenye gari, wakikimbiza na wanyama wachanga kwa gari, kuruhusu watoto wadogo kuwapiga risasi wanyama na kukamata mnyama mdogo na kuanza kumtesa huku kichanga kikipiga kelele na kujaribu kukimbia bila mafanikio.

Utakachoona ni kama vile wawindaji hao wanawinda ndani ya uani wao bila wasiwasi wowote. Motherboard imejaribu kuwasiliana na Nyalandu na Msigwa lakini hawaku-respond, lakini mwakilishi wa Green Mile alisema kuwa serikali na Dallas Safari Club ndiyo wa kulaumiwa kwa unyanyasaji huu wa wanyama.

Green Mile Safari Co Ltd wanashangaa kwa nini unyanyasaji huo ulitokea mbele ya maafisa wa serikali. Wanadai kinachoitwa unyanyasaji wa wanyama kama kinavyoonekana kwenye video hapo chini ni mpango wa wapinzani wao kutoka Marekani kwamba hawashangai kwa kwa Nyalandu kuwasifu Dallas Safari Club baada ya kuwaadhibu Green Mile safari Ltd:

Leaked Animal Abuse Video Shows Everything That's Wrong with Big Game Hunting | Motherboard