Kama
unataka kujua hoteli bora za Afrika, tuzo za hivi karibuni za Reader’s
Choice Awards zilizoandaliwa na kampuni ya Condé Nast Traveler zinaweza
kukupa jibu.
Muonekano wa nje wa Gibb’s Farm, Ngorongoro
Cape Town, South Africa imeongoza kwa kuwa na hoteli tano kwenye orodha ya hoteli 10 zilizotajwa.
Gibb’s Farm
Gibb’s
Farm, Ngorongoro, Tanzania imekamata nafasi ya sita. Mwaka huu wasomaji
76, 659 wamejibu questionnaire zilizoandaliwa kubaini hoteli bora.
Chumba kimoja wapo katia ya 16 vilivyopo
Kipengele kingine kwenye tuzo hizo ni Top 20 Safari Lodges & Camps
ambapo Tanzania zimeingia mbili. Singita Grumeti ya Serengeti imekamata
nafasi ya tatu na Four Seasons Safari Lodge Serengeti imekamata nafasi
ya 8.