Na Walter
Mguluchuma
Mpamda Katavi
Maadhimisho ya Siku ya Chakula
Duniaani ambayo hufanyika kila
mwaka Oktoba 16 yamepanga kuadhimishwa Kitaifa Mkoani Katavi kuanzia
Oktoba 13 hadi hadi oktoba 16 katika
uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dr Rajabu Rutengwe
wakati alipokuwa akitowa taarifa
ya maadhimisho ya hayo hapo jana
mbele ya waandishi wa ofisini
kwake
Alisema katika
kuadhimisha siku hiyo Mkoa wa Katavi umefanya
maandalizi ya kutosha
ilikuweza kuwaonyesha wananchi
mbalimbali yale yanayofanyika katika sekta ya kilimo
mifugo ,nyuki na ushirika
Dr Rutengwe
alisema kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na maonyesho ya badhaa mbalimbali zinazohusiana
na sekta ya kilimo
Alifafanua wageni watakao toka nje ya Mkoa wa
Katavi watapata furusa ya kutembelea
miradi mbalimbali ya sekta ya
kilimo kwa lengo la kujifunza
yanayofanyika katika Mkoa wa Katavi na
iliwaweze kutowa ushauri wa namna
ya kufanikisha zaidi
utendaji wa kazi katika sekta ya kilimo katika Mkoa wa Katavi
Mkuu wa Mkoa Dr Rutengwe alieleza kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na kongamano
na kilimo litakalo jadili masuala
ya Hifadhi ya mazao ,uongezaji wa
thamani ya mazao,uboreshaji wa kuku wa asili na utunzaji wa mazingira
pamoja na uboreshaji wa lishe
katika Mkoa wa Katavi
Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kuitumia furusa hii
ipasavyo kwa lengo la kujifunza na kuhakikisha yale watakayojifunza wayatumie vizuri
na kwa usahihi zaidi ili
kuweza kubadilisha hali ya kilimo
na maisha kwa ujumla
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni kilimo cha Kaya lisha Dunia
tunza mazingira hivyo Mkuu huyo
wa Mkoa ametaka kaulimbiu hii iende sambamba na kauli mbiu ya Mkoa wa Katavi isemayo Katavi bila umasikini inawezekana
Mwisho