Kiwanja
cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam
Tanzania (DAR), kimetajwa katika orodha ya viwanja vya ndege vilivyo
vibaya zaidi barani Afrika kwa mwaka 2014.
Picha kwa hisani ya Roland, http://www.flickr.com/photos/43532166@N00/4745639378 |
Kwa
mujibu wa matokeo ya utafiti ulioendeshwa na mtandao wa
www.sleepinginairports.net, uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam unashika
nafasi ya nne (4) kwa ubaya ukitanguliwa na kiwanja cha ndege
cha Khartoum International Airport, Sudan (KRT),Kinshasa N’djili
International Airport, Democratic Republic of the Congo (FIH),
na Tripoli International Airport, Libya (TIP). Utafiti huo hufanyika kwa
kukusanya kura zinazopigwa kutoka kwa wasafiri mbalimbali ambao kwa
ujumla wana uzoefu wa safari za anga.
Ifuatayo ni orodha kamili ya viwanja 10 vibaya zaidi barani Afrika kwa mwaka 2014;
- Khartoum International Airport, Sudan (KRT)
- Kinshasa N’djili International Airport, Democratic Republic of the Congo (FIH)
- Tripoli International Airport, Libya (TIP)
- Dar es Salaam Julius Nyerere International Airport, Tanzania (DAR)
- Luanda Quatro de Fevereiro International Airport, Angola (LAD)
- Port Harcourt International Airport, Nigeria (PHC)
- Abuja Nnamdi Azikiwe International Airport, Nigeria (ABV)
- N’Djamena International Airport, Chad (NDJ)
- Accra Kotoka International Airport, Ghana (ACC)
- Lagos Murtala Muhammed International Airport, Nigeria (LOS)
Miongoni mwa sababu zilizochangia hali mbaya ya viwanja hivi ni kuanzia
- sakafu chafu,
- vyoo na mabafu machafu
- maombi ya mara kwa mara ya rushwa
Kwa ujumla abiria hawaridhishwi na huduma zitolewazo katika viwanja hivi.
Malalamiko
mengine ya abiria ni juu ya hali mbaya ya hewa (hakuna vipooza joto),
pia mparaganyiko wa safari za ndege (safari huvurugika mara kwa mara),
uhaba wa huduma za mgahawa (iliyopo ni michache na hutoa huduma kwa
gharama za juu sana), huduma za usalama zisizo aminika.
Wasafiri
wengi kupitia viwanja hivi vya ndege hukwepa kukutana na hali
itayowalazimu kulala katika viwanja hivyo na iwapo itawalazimu kulala,
hutafuta huduma ya hoteli za karibu kuliko kulala katika viwanja hivyo
vya ndege.
Iwapo
itakutokea kukwama katika viwanja hivyo kutokana na kucheleweshwa kwa
safari yako, jiandae kuwa mvumilivu kabisaa kwa hali utazokutana nazo.