Sehemu ya wafanyakazi wa shirika la bima makao makuu toka idara za fedha
na utawala wamefanya ziara ya utalii wa ndani katika masalio ya
historia na mambo kale ya mji wa Bagamoyo Jumamosi ya oktoba 25 ili
kujifunza mambo ya historia ya zamani.
Katika
ziara hiyo Wafanyakazi hao wametembelea kijiji cha kaole ambacho kuna
makaburi ya watu mashuhuri na kumbukumbu za kihistoria. Pia walipata
nafasi ya kutembelea mji mkongwe wa Bagamoyo wenye majengo ya kale
yaliyokuwa ngome za tawala za kikoloni ambapo pia majengo hayo
yalitumika kama jela za kikoloni, na bandari ya kusafirisha watumwa
katika karne zilizopita.
Aidha ziara hiyo iliwapeleka hadi katika kanisa la kwanza la Romani
katoliki ambalo hapo ndipo ulipohifadhiwa mwili wa mgunduzi wa mambo ya
historia Dkt. Livingstone kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Scotland kwa
mazishi.
Kanisani
hapo ndio sehemu ya kwanza kuzaliwa kuenea kwa ukristo katika nchi ya
Tanganyika na sehemu nyingine.
Wafanyakazi hao wamepata wasaa wa kuitembelea iliyokuwa bandari ya
Bagamoyo na soko maarufu la samaki na kujionea wakazi wa Bagamoyo
wakijishungulisha na kazi za uvuvi wa samaki na uuzaji wa vitu vya asili
na utamaduni vya kitanzania.
Akiongelea
safari hiyo mkurugenzi wa fedha na utawala wa shirika hilo Anna
Mbughuni amesema wamekuja kujifunza mambo ya historia na kuitumia ziara
hiyo ili kujenga mshikamano miongoni mwa wafanyakazi na kuongeza tija.
”
tumekuja hapa tubadilishane mawazo na kupeana hamasa ya kutimiza
majukumu yetu, Pia ni fursa ya wafanyakazi kupumzika na kufurahi pamoja
baada ya kufanyakazi kwa kipindi kirefu”anasema mkurugenzi huyo.
”ziara
hizi zinaongeza ari kwa wafanyakazi, ona leo tumejumuika pamoja toka
idara tofauti bila ubaguzi wala hadhi sote hapa ni kitu kimoja wenye
malengo yanayofanana juu ya shirika letu la bima”anamaliza kusema mkuu
huyo wa fedha.
Naye
meneja utumishi wa shirika hilo Godbless Uronu amesema wamekuja
Bagamoyo kufanya utalii wa ndani na kujenga mahusiano mema na
ushirikiano miongoni mwao kwani ufanisi bora kazini huenda pamoja na
mshikamano.
”lengo
letu pia kujitangaza kibiashara kwa wateja walioko nje Dar es salaam
kwa hiyo kupitia ziara hizi tunapata fursa ya kukutana na watu
mbalimbali.”anasema meneja huyo
”tumekuja kama sehemu ya kujifunza mambo ya historia pia tunaitumia siku
hii kubadilishana mawazo na kuhamasisha mashirika mengine yaweze
kufanya shughuli za utalii wa ndani”anamaliza meneja utumishi wa shirika
hilo.
Baadhi
ya wafanyakazi wamesema wamekuja Bagamoyo kujionea yale mambo ya
kihistoria ambayo wameyasoma katika vitabu.kupitia ziara hiyo wamepata
fursa ya kujua uzuri unaozungumzwa kuhusu Bagamoyo na mambo ya kale
yaliyopata kutokea huko siku za nyuma.
“ndio
mara yangu ya kwanza kuja Bagamoyo nimefurahi nimejifunza mengi na
nimeona mengi nawaomba watanzania wenzangu wawe na mazoea ya kutembelea
sehemu za utalii, bila kungoja wageni waje kutembelea,” anasema
mfanyakazi wa shirika hilo
Bagamoyo
ni miongoni mwa masalia ya kihistoria ambapo palikuwa mashuhuri kwa
biashara ya watumwa waliosafirishwa na wakoloni kwenda kufanya kazi
katika mashamba na viwanda nje ya bara la Afrika.