Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu wa pili kulia), Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi ( wa kwanza kulia) wakiwa
katika sala kabla ya kuanza Mkutano aa Viongozi wa dini zote nchini
kushirikiana kwa pamoja kupambana na ujangili wa Wanyamapori na
usafirishaji haramu wa Wanyamapori hai, Wengine ni Rais wa Baraza la
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa ( wa kushoto) akifuatiwa na Waziri kivuli wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa
Waziri wa Maliasili na Utalii imeanza kushirikiana na viongozi wa
dini nchini katika kuhakikisha kuwa ujangili wa Wanyamapori , biashara
ya meno ya tembo na usafirishaji haramu wa wanyamapori hai unakoma kwa
kuwaelimisha Viongozi wa dini zote nchini ili waweze kuwahuburia
waumini wao kuacha kujihusisha na vitendo hivyo kwani ni chukizo mbele
ya Mwenyezi Mungu.
Akizungumza kwenye mkutano wa Viongozi wa
dini zote nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam Mhe, Nyalandu
alisema vita dhidi ya Ujangili vinahitaji ushirikiano wa pamoja hasa
kwa viongozi wa kiroho kwani wao wana kundi kubwa la watu
wanaloliongoza katika jamii kwa kuwahudumia kiroho na kimwili.
Mkutano huu ni moja ya maazimio yaliyofikiwa mwezi wa tano huu kwenye
mkutano mwanzo uliofanyika jijini Dare s Salaam wa kujadili mikakati ya
kutokomeza ujangili wa wanyamapori na biashara ya meno ya tembo
uliohusisha Wizara ya Maliasili na Utalii, Wadau wa Kimataifa wa
Maendeleo na Jumuiya za kimataifa ikiwepo UNDP NA ICCF.
Mhe.
Nyalandu alisema Viongozi wa dini ni watu muhimu sana katika
kuhakikisha Maliasili za taifa ikiwemo wanyamapori na misitu inalindwa
na kuhifadhiwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa hata
vitabu vitakatifu na kurani vinasisitiza umuhimu wa kulinda na kuhifadhi
viumbe vya Mwenyezi Mungu.
‘’Viongozi wa dini lazima muwahubuirie waumini wenu kuwa kujihusisha na ujangili ni dhambi hivyo lazima waaachanae na vitendo hivyo viovu’’ Mhe. Nyalandu alisema
Alisema watu wanaojihusisha na mauaji ya tembo na usafirishaji haramu wa wanyamapori hai ni waumini wa dini ya kikiristo na dini ya kiislaamu hivyo kama Viongozi wa dini wakikemea vitendo hivyo viovu makanisani na misikitini kwa kuwakanya waumini wao hivyo wataweza kuachana na vitendo vya ujangili.
‘’Viongozi wa dini lazima muwahubuirie waumini wenu kuwa kujihusisha na ujangili ni dhambi hivyo lazima waaachanae na vitendo hivyo viovu’’ Mhe. Nyalandu alisema
Alisema watu wanaojihusisha na mauaji ya tembo na usafirishaji haramu wa wanyamapori hai ni waumini wa dini ya kikiristo na dini ya kiislaamu hivyo kama Viongozi wa dini wakikemea vitendo hivyo viovu makanisani na misikitini kwa kuwakanya waumini wao hivyo wataweza kuachana na vitendo vya ujangili.
Aidha, alisema kuwa kupitia mkutano huo,
Serikali pamoja na viongozi wa dini watakuwa na sauti moja yenye nguvu
ambayo waumini wa dini zote wataweza kuisikia na kuitekeleza katika
mapambano ya kuhakikisha mauaji ya tembo na usafirishaji haramu wa
wanyamapori hai unakoma kwa kuwa Viongozi wa dini ni watu wenye sauti
yenye kugusa mioyo ya watu.
Aliongeza kuwa, Viongozi wa dini
kupitia mkutano huo sio tu watashiriki kwenye vita dhidi ya Ujangili pia
watakuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya uhifadhi na uendelezwaji wa
Maliasilli za taifa.
‘’Sauti za viongozi wa dini ni kubwa
kuliko bunduki na ni kubwa kuliko magereza hivyo tunaamini Maliasili za
taifa zitaendelea kulindwa na kuhifadhiwa kwa kushirikiano nao.’’ Mhe
Nyalandu alisitiza
.
Naye , Shekhe wa Dar es Salaam ,Alhadi Musa Salumu alisema wamenyamaza kiasi cha kutosha huku vitendo viovu vikiendelea kutafuna Maliasili za Taifa hivyo ni lazima wasimamie uadilifu na hisani sio kwa binadamu tu hata kwa viumbe wengine wakiwemo Wanyama pamoja na ndege nao wanahitaji hisani ya kuishi katika mazingira yao kwa kutendewa wanavyostahili.
.
Naye , Shekhe wa Dar es Salaam ,Alhadi Musa Salumu alisema wamenyamaza kiasi cha kutosha huku vitendo viovu vikiendelea kutafuna Maliasili za Taifa hivyo ni lazima wasimamie uadilifu na hisani sio kwa binadamu tu hata kwa viumbe wengine wakiwemo Wanyama pamoja na ndege nao wanahitaji hisani ya kuishi katika mazingira yao kwa kutendewa wanavyostahili.
‘’Mwenyezi Mungu
anasema kila kitu kitendewe wema hata mnyama anayestahili kuuawa sio
lazima umpige risasi kumi na moja wakati kulikuwa na uwezekano wa
kutumia risasi moja tu’’ Shekhe Salum alisema.
Alibainisha kuwa
Wanyama wana haki ya kufurahia mazingira yao kama Mtume anavyowataka
waislamu wawetendee uadilifu na hisani wanyama wote wanaoliwa na
wasioliwa na sio uharamu wanaofanyiwa sasa baadhi ya Wanyamapori kwa
kuwaua na kuwang’o pembe na meno yao.
Naye,Rais wa Baraza la
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa alisema Mungu kampa Binadamu uwezo wa kuvitawala viumbe
vyote vinavyopatikana katika uso wa dunia na sio kuvipukutisha kama
wanavyofanya sasa kwani hayo sio mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Amesema tani za magogo pamoja na biashara ya meno ya tembo zinazoendelea
kusafirishwa kila kukicha ni ishara tosha kuwa baadhi ya watu hawana
hofu ya Mungu hivyo wao kama viongozi wa kiroho wataendelea kuwaelimisha
waumini wao na ikiwezekana kuwakemea kwani kuna binadamu wenye macho
lakini hawaoni na kuna binadamu wenye masikio lakini hawasikii.
Alisema Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa dini ni lazi
wahakikishe Chama cha Haki za wanyama kinafufuliwa kwani kwa sasa
Wanyama wanoishi majumbani na wanyamapori wamekuwa wakimbuna na ukatili
usiovumilika hivyo lazima watetewe.
Aidha, Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi alisema kuwa mkutano huo ni muhimu
sana kwani Watumishi wa Mungu ni watu wanaoaminika katika jamii na
wanajukumu kubwa sana katika kuhakikisha viumbe vyote vilivyoumbwa na
Mwenyezi Mungu vinaendelea kuwepo kwa ajili ya kizazi cha sasa na
kijacho.
Amesema Viongozi wa dini ni lazima wawe thabiti katika
vita dhidi ya Ujangili wa wanyamapori, Biashara ya meno ya tembo na
usafirishaji haramu ya Wanayamapori hai kwani kwa sasa hali inatisha na
wahusika ni wanaojishughulisha na vitendo hivyo ni Waumini wa dini zote
za kikiristo na kiislamu.
‘’ Watumishi wa Mungu na sisi wafuasi
wenu lazima tutambue Maliasili ni mali za Mwenyezi Mungu na ametupa
mamlaka ya kuzitumia na si kuzimaliza kama tunavyofanya sasa hatuna
haki hiyo sisi tumezikuta basi tusizitumie kwa fujo’’
Alisema Watumishi wa Mungu wana kazi kubwa ya kuwaonesha na kuwafundisha Waumini wao kuwa Mapenzi ya Mungu yanawataka watunze viumbe alivyoumba Mwenyezi Mungu na sio kuviharibu kwani hizo ni zawadi walizopewa na Mwenyezi Mungu’’
Alisema Watumishi wa Mungu wana kazi kubwa ya kuwaonesha na kuwafundisha Waumini wao kuwa Mapenzi ya Mungu yanawataka watunze viumbe alivyoumba Mwenyezi Mungu na sio kuviharibu kwani hizo ni zawadi walizopewa na Mwenyezi Mungu’’
Amesema kama viongozi wa dini
wakiweza kufikisha ujumbe kwa waumini wao vita hivi vitafanikiwa kwa
sababu wanaaminika kwenye jamii na wana nguvu kubwa sana kwa jamii
hivyo chochote wanachosema wanaaminika kwa jamii kwa sababu Waumini wa
dini zote wanazungumza na Mungu kupitia wao.
‘’ Viongozi wa dini
tuonesheni njia katika hili , tukeemeeni pale mnapoona hatuendi sawa
kama mnaamini tunayofanya sio mapenzi ya Mwenyezi Mungu ’’ Dkt. Mengi
alisisitiza
Naye Waziri kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa ifike hatua sasa viongozi wa dini
wakatae michango ya pesa ya watu wanaotaka kujenga makanisa kwa pesa
walizozipata kupitia ujangili wa Wanyamapori kwani kufanya hivyo ni
kuhalalisha ujangili kwenye nyumba za ibada.
Akiwa na kofia mbili
ya uchungaji na pia ni mwanasiasa amewataka viongozi wa dini
kutowanyamzia wanasiasa wanapokengeuka kwa kuhamasisha wananchi kuharibu
maliasili za taifa kwa mtaji wa kura hivyo ni lazima wa wakemee kwa
nguvu zao zote bila kujali cheo na hadhi ya wanasiasa hao pindi
wanapofanya hivyo.
Pia amesema suala la kupambana na ujangili
halina chama wala itikadi hivyo amewataka viongozi wa dini kulikemea
kwenye nyumba za ibada kwani viongozi wa dini watu wenye nguvu na
wanaoheshimika katika jamii.