Na Abdulaziz Ahmeid-Dodoma
Wanasiasa
wameombwa kutoa ushirikiano kwa taasisi na wadau mbalimbali
wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu na mazingira badala ya wao kuwa ni
miongoni mwa watu ambao wanaoshiriki na kusababisha uharibifu wa
mazingira unaondelea kwa kasi hapa nchini.
Wito
huo umetolewa leo mjini Dodoma na mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa
jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania(MJUMITA)Bi Rahima Njaidi Wakati wa
ufunguzi wa warsha na mkutano mkuu wa 14,ambao umeshirikisha wanachama
wajumuia hiyo na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu
na mazingira toka kanda sita Nchini.
Bi
Njaidi alibainisha kuwa ili kufaniwa katika mapambano na harakati za
kuhifadhi misitu na mazingira ni wajibu kwa wanasiasa kushirikiana na
taasisi mbalimbali zilizopo katika mapambano na harakati hizo zenye
lengo la kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi nakutishia
‘ kupitia mpango huo Wanajamii wamediriki kuwahoji viongozi wao katika
mchakato mzima wa usimamizi endelevu wa rasilimali misitu ambapo suala
la Mapato ya vijiji vya uhifadhi ni moja ya changamoto iliyoonekana
katika warsha hii’ alibainisha Njaidi
Akimalizia
taarifa yake katika warsha hiyo Njaidi aliviomba vijiji kuachana na
baadhi ya wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wana katika jamii na pia ni
washiriki wakubwa uharibifu wa misitu na mazingira kwa kuwaruhusu
wananchi wanaowaongoza kuishi na kufanya shughuli za kibinadamu
zinazoharibu maliasili kwa lengo la kuwafurahisha wanaowaongoza au kwa
maslahi binafsi
Nae Bw Musa Mkoyage,
Diwani
wa kata ya Likongowele wilayani Liwale aliitaka MJUMITA iwaelimishe
wanajamii juu ya ugawanaji wa mapato kama vile ilivyoainishwa katika
vijiji vingine ambavyo tayari vimeishaanza kupata faida za misitu huku
mapato yote yakibaki kijijini na kuweza kuendeleza shughuli mbali mbali
za maendeleo.
Mkoyage
pia alieleza kuwa katika kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi na
kutishia uwepo wake hapa nchini na kusababisha hofu ya nchi kugeuka
jangwa
Akifungua Warsha hiyo ya siku mbili,Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Bw Lefy
Gembe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Bi Chiku Galawa Aliwataka
wajumbe wa mkutano huo kufanya tathmini ili kujua ni kwa kiasi gani
taratibu na kanuni za uvunaji endelevu zinasimamiwa na kufanikiwa ili
kila mwananchi ashiriki kulinda na kuhifadhi misitu na mazingira kwa
manufaa ya jamii
‘Uvunaji endelevu ni suala la kisheria hivyo ni muhimu kwa wananchi
kutekeleza taratibu na sheria zilizopo ili misitu iweze kuwa endelevu na
Iwe yenye tija kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Warsha
hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa MJUMITA na kushirikisha wadau
mbalimbali ikiwemo Jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF) ikiwa na lengo
kuu la kutafuta mbinu za kupambana na uharibifu wa misitu na mazingira
na kufanya usimamizi na uvunaji endelevu
kutoka
kulia ni mkurugenzi wa Mjumita Bi Rahima Njaidi;Afisa Mtendaji Mkuu wa
shirika la Mpingo Bw Gasper Makala;mkurugenzi wa Tfcg na mwanamtandao
wakijadili jambo kuhusiana na uhifadhi wa misitu
Washiriki katika warsha
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Lephy Gembe akiongea kwemye warsha hiyo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mjumita,Bi Rahima Njaidi akitoa utangulizi wa warsha ya ya
siku mbili ya wadau wa mtandao huo inayoendelea Mkoani Dodoma
Mkuu wa wilaya Dodoma(suti nyeusi)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Mjumita