Picha: Mabonge ya Barafu (mawe) yaliyoua watu Kahama

Watu 38 wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo... thumbnail 1 summary
Watu 38 wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi walelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine watatu wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.


Amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.


 

Akiwa eneo la tukio Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo.