MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI MIRISHO SARAKIKYA APEWA TUZO YA HESHIMA NA TANAPA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MARA 38

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akimkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Sarakikya akiwa ... thumbnail 1 summary
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akimkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerali Sarakikya pia  amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake, lakini katika hatua nyingine  atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani  yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa  mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerali Mirisho Sarakikya  amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo  ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wamepewa tuzo hizo. Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
Meneja  wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy Sikagonamo mwandishi bora wa  habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa  mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten  Morogoro, mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mlimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro  kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti  katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga  mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.