Mwakilishi
wa Ufaransa katika UNESCO, Jean-Pierre Poncet akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum
uliofantika leo makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa
RoadToParis with tabianchiblog&CFIMedias21
Mwakilishi
wa Ufaransa katika UNESCO, Jean-Pierre Poncet amesema kuwa,
Maaendeleo endelevu hayatapatikana bila kutatua changamoto za mabadiliko
ya tabianchi ambayo yanazikumba nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania na
nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Mwakilishi huyo ameeleza hayo leo Julai 6, wakati akizungumza na waandishi wa habari
za mazingira kutoka Tanzania, Kenya, Madagascar na Rwanda wanaoshiriki
kwenye mkutano mkuu wa wanasayansi juu ya tabianchi ‘Our Common Future
Under Climate Change’ unaotarajia kuanza rasmi Julai 7-11, katika makao
makuu ya UNESCO, jijini Paris, Ufaransa.
Anasema
kuwa, ili nchi ziwe na maendeleo, suala la kupambana na mabadiliko ya
tabianchi ni muhimu kuweka mipango madhubuti yatakayoendana na mipango
yao ya maendeleo.
Kuelekea
katika mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya
tabainchi (COP 21) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu,
Paris.
Anasema kuwa ili kuleta maedeleo na kupambana kwa vitendo, ni wajibu kwa mtaifa kutoa
mchango wao katika juhudi za dunia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Intended
Nationally Determined Contributions – INDCs).
Waandishi
wanaoshiriki katika mkutano huo wa wanasayansi unaotarajia kuanza
kesho, awali ndani ya mwezi Juni, walipatiwa mafunzo ya wiki mbili
Nairobi, Kenya juu ya mabadiliko ya tabianchi chini ya mradi wa Media 21 Project.
Mwakilishi wa Ufaransa katika UNESCO, Jean-Pierre Poncet akiwa katika mkutano na waandishi wa habari
Mwakilishi
wa Madagascar, mwanahabari/blogger, Lalatiana Rahariniaina akiwa katika
pozi... nje ya eneo la kuingilia ukumbi wa mikutano ambao unatarajia
kuanza kuanzia Julai 7-11, UNESCO, Paris.Mwandishi wa mtandao wa habari wa modewjiblog.com,
Andrew Chale akiwa katika eneo la kuingilia kwenye mkutano katika
makao makuu ya UNESCO, Paris tayari kwa mkutano unaotarajia kuanza kesho
Julai 7-11.
Chanzo: Moblog