Dr
Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa
kwake huku Kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za
wizara hiyo.
Mwanamitindo
wa Kimataifa anaefanyia kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata
amechagulia na Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Balozi wa Hiyari ‘Good
Will Ambassador’ kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza
vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Flaviana
ambaye juzi alikuwa mmoja kati ya shuhuda wa kushuhudia Wizara ya
Maliasili na Utalii wakizindua rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza
vivutio vya Tanzania nje ya anchi alitawazwa leo hii na Katibu Mkuu Dr
Adelhelm James Meru aliyemkabidhi kwa niaba ya Waziri, Mheshimiwa mwenye
dhamana Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi Madam Devota Mdachi
akishuhudia.