Mjadala: Mipaka ya nchi na nchi haihamishiki? Je, tuilinde au tuiache wazi?

Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mambo ya Ushirikiano na Utamaduni, Ubalozi wa Ufaransa, Philippe Boncour, Mkurugenzi wa Shirika la... thumbnail 1 summary
Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mambo ya Ushirikiano na Utamaduni, Ubalozi wa Ufaransa, Philippe Boncour, Mkurugenzi wa Shirika la Kusaidia Wakimbizi la Asylum Access Tanzania, Janemary Ruhundwa, Profesa Michel Foucher, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mipaka na balozi wa zamani wa Ufaransa, Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Joyce Mends-Cole na Profesa Bonaventure Rutinwa, kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Slaam.
 Wageni waalikwa wakifuatilia mjadala huo
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak akifungua mjadala huo ambao ulihudhuriwa na watu kutoka mataifa mbalimbali

Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni na lugha Alliance France, Septemba 17 kimeendesha mjadala mkubwa kujadili faida na madhara ya kuwa na mipaka kati ya nchi na nchi, bara kwa bara. 

Mjadala huo uliolenga kujadili kauli hii “Mipaka haihamishiki? je tuilinde au tuiache wazi?, uliongozwa na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Ushirikiano na Utamaduni, Ubalozi wa Ufaransa, Philippe Boncour na kuwashirikisha wachangia mada akiwemo Profesa Michel Foucher, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mipaka na balozi wa zamani wa Ufaransa.

Wengine ni mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Joyce Mends-Cole, Mkurugenzi wa Shirika la Kusaidia Wakimbizi la Asylum Access Tanzania, Janemary Ruhundwa, na Profesa Bonaventure Rutinwa, kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Slaam.

Awali akifungua mjadala huo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak alielezea umuhimu wa majadilino hayo hasa katika wakati huu ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji duniani.

Ripoti kamili ya yaliyojiri kuhusu mjadala huu itakujia hivi karibuni…