Kiongozi wa msafara wa wanamazingira waliotembea kwa miguu wakiokota
taka za plastiki pembezoni mwa barabara kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro
na kuja jijini Dar es Salaam, Felix Garbe (kushoto) akimkabidhi ufagio
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo Kibo Dar es Salaam, Sophia
Yusuf ikiwa ni ishara ya kuhamasisha wakazi wa Dar es salaam kuchukua
jukumu la kutunza mazingira. Tukio hilo lilifanyika baada ya
wanamazingira hao kuwasili jijini Dar es Salaam baada ya safari
iliyowachukua muda wa wiki tano kumalizika.
(Picha: Hisani ya Nipe Fagio)