Na Mwandishi Maalum, New York
Zaidi
ya nchi 162 zinatarajiwa kutia saini leo ( Ijumaa) Makubaliano kuhusu
mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yalifikiwa jijini Paris -Ufaransa
mwezi Desemba Mwaka jana.
Miongoni
mwa nchi ambao zimethibitisha kushiriki hatua hiyo muhimu na ambayo
ni hatua ya mwanzo kuelekeza utekelezaji wa makubaliano hayo maarufu
kama Paris Agreement ni pamoja na Mataifa makubwa kiuchumi duniani
na ambayo yanachangia kwa asilimia kubwa katika utoaji wa hewa ya
ukaa.
Baada
ya utiaji saini wa makubaliano hayo katika mkutano ambao umeandaliwa
na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, nchi wanachama wa
Paris Agreement watatakiwa ama kupitisha makubaliano hayo au
kuridhia ( ratification).
Ili
hatua ya utekelezaji ianze Nchi 55 zinatakiwa kuridhia makubaliano
hayo ndani ya siku thelathini, na nchi hizo 55 zinatakiwa ziwe ni
zile ambazo kwa ujumla wake zinachangia asilimia 55 ya hewa ukaa.
Taarifa
kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa zimeeleza kuwa mataifa
makubwa kama Marekani na China yameonyesha nia ya kutia saini
makubaliano hayo huku nchi ndogo na zinazoendelea zipatazo 13
zinatarajiwa kusaini na kuridhia makubaliano hayo.