Kikundi cha Vijana Wajasiriamali katika mradi wa kutunza mazingira chawezeshwa

Airtel Fursa imewapatia pikipiki mbili aina ya Guta, na vifaa vya kufanyia usafi kwa kikundi cha Pambana Dodoma, Jumapili 1 Mei 2016, Pa... thumbnail 1 summary
Airtel Fursa imewapatia pikipiki mbili aina ya Guta, na vifaa vya kufanyia usafi kwa kikundi cha Pambana

Dodoma, Jumapili 1 Mei 2016, Pambana ni kikundi cha vijana 30 wajasiriamali kinachojishughulisha na shughuli mbalimbali katika jamii kama kukusanya taka, kuzalisha na kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini Dodoma, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi, mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na vifaa vingine vya usalama vya kufanyia kazi zao.

Afisa uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa juhudi zao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, " Tumeamua kutoa vitendea kazi vya usafi ili kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia lengo kuu la kuhakikisha maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya usafi na hivyo kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla. Sambaba na hili Airtel imeona nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na kukuza biashara yao".

"Kikundi cha Pambana kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Kaniki."Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao." alisema Kaniki.

Kwa upande mwingine kundi la Pambana waliahidi kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi.Kiongozi wa kikundi hicho, Amasha Zuberi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana zaidi katika Jamii.

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo Majengo jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.