TAMISEMI Pamoja na TNRF waendesha mafunzo kwa waandishi wa habari leo mjini Dodoma

 Mratibu wa Mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi Tanzania  (DCFP), TAMISEMI, Sanford Kway akitoa mafunzo kwa wanahabari wa mabadilik... thumbnail 1 summary
 Mratibu wa Mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (DCFP), TAMISEMI, Sanford Kway akitoa mafunzo kwa wanahabari wa mabadiliko ya Tabianchi pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira walofika kwenye semina iliyofanyika katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.

Mkutano ukiendelea 
  Mratibu, Mawasiliano na uchechemuzi Jumuiko la Maliasili Tanzania, Sophia Masuka akitolea ufafanuzi kuhusu kazi za taasisi ya TNRF inavyoshirikiana na serikali kupitia TAMISEMI ili kuweza kupambana na mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.
Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Paul Dotto Kuhenga akitoa mada kwa waandishi wa habari pamoja na wadau wa Tabianchi kuhusu mabadiliko ya Tabianchi na jinsi ya waandishi wa habari  kuandika habari zinazohusiana na mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza mabadiliko hayo'
Salehe Msanda kutoka TAMISEMI akichangia mada kuhusiana na miradi inayotarajiwa kuanzishwa katika Wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro katika mafunzo hayo yanayoendelea leo mkoani Dodoma katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Ofisi ya makamu wa raisi 
Mwandishi wa habari kutoka (TBC)Akiwa anauliza swali katika mafunzo yanayoendelea leo Dodoma
Picha ya pamoja

Asasi ya kiraia ya Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) kwa kushirikiana na Ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi)wameandaa mafunzo Kwa waandishi wa habari,Maafisa mawasiliano na Tehama kutoka kwenye idara za serikali kuhusu mradi wa kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo mratibu wa Mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi Tanzania(DCFP) ambaye pia ni Afisa misitu mkuu Tamisemi Sanford Kway amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitano unaolenga kuwekeza kwenye miradi ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika halmashauri 15 ambapo Kwa sasa unafanyika Kwa majaribio katika halmashauri 3 ambazo ni Monduli, Longido na Ngorongoro .

Halmashauri hizo nyingine ni Pamoja na Zanzibar (Micheweni,Unguja Kaskazini A na Unguja Kusini)ambapo kwa Tanzania bara ni wilaya 15 ambazo ni Bahi, Iramba, Kilwa, Kiteto, Kondoa, Longido ,Manyoni, Mbulu, Mpwapwa, Monduli, Ngorongoro, Pangani, Same, Siha na Simanjiro.

Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza umeanza mwaka 2016 -2018 ambapo upo chini ya Uratibu wa jumuiya ya Kimataifa ya Mazingira na maendeleo (IIED)unahusisha halmashauri za Wilaya (3) ambazo ni Monduli,Longido na Ngorongoro

Aidha amesema kuwa awamu ya pili ya mradi huo utakuwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) na itahusisha halmashauri za wilaya 12o zilizosalia.