WADAU WA KAMPENI YA MAMA MISITU WAJADILI NAMNA YA KUENDELEZA USIMAMIZI NA UTAWALA BORA WA MISITU HAPA NCHINI

 Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Dr. Suma Kaare akitoa historia ya kampeni ya Mama Misitu tangu iliyoanzishwa... thumbnail 1 summary
 Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Dr. Suma Kaare akitoa historia ya kampeni ya Mama Misitu tangu iliyoanzishwa mwaka 2008 mpaka 2017 kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Misitu  uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam leo tarehe 29/09/2017.
 Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Zakaria Faustin akiwakaribisha wadau mbalimbali wa Misitu waliokuwa kwenye kampeni ya Mama Misitu pamoja na kutoa mutasari wa kampeni ya Mama Misitu kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maliasili, Misitu na Nyuki, Seleboni John Mushi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akuzungumzia namna serikali kupitia wizara hiyo wanavyoshirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusiha kwenye masuala ya usimamizi wa masaula ya misitu pamoja na kuwa bega kwa bega ili kuweza kulinda misitu iliyopo hapa nchini.
 Mratibu wa Miradi ya Maliasili kutoka Ubalozi wa Finland nchini Tanzania, William Nambiza akizungumza kuhusu namna ubalozi wa Finland nchini Tanzania ulivyosaidia kudhamini kampeni ya Mama Misitu toka mwaka 2008 mpaka mwaka 2017
Mwakilishi wa Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Kari Leppanen akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa video fupi ya technolojia ya kisasa ya kuchakata Magogo ambayo imetengenezwa na kampeni ya mama misitu kwa kushikirikiana na Panda Miti Kibiashara. 
 Mwakilishi wa Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Kari Lepanen akizungumza kuhusu mchango wa Ubalozi wa Finland ulivyosaidia kusimamia kampeni ya Mama Misitu wakati wa kufunga kampeni hiyo.
 Balozi wa Kampeni ya Mama Misitu, Asha Mshana akitoa igizo kwenye mkutano wa kufunga kampeni ya Mama Misitu uliowakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili namna ya kuendeleza miradi mingine inayohusu usimamizi wa maliasili hasa misitu hapa nchini Tanzania. Katika igizo hilo Mama misitu alitoa kauli mbiu yake "Misitu ni uhai nani Maisha yetu, hivyo kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe anaitunza na kuilinda misitu yetu kwa faida yetu na vizazi vyetu"
 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano.-Jumuiko la Maliasili Tanzania,Sophia C. Masuka pamoja na aliyekuwa  Meneja wa kampeni ya Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala wakiangalia video fupi inayoelezea teknolojia ya kisasa ya kuchakata magogo. Video hii inatarajia kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya television kuanzia mwezi wa kumi 2017. 
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Misitu waliokuwa kwenye kampeni ya Mama Misitu wakifuatilia mada kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili namna ya kusimamia misitu mara baada ya kampeni ya Mama Misitu kumalizika hapa nchini
 Afisa Programu wa Policy Forum, Prisca Kowa akitolea ufafanuzi kuhusu dhana ya Uwajibikaji Jamii(SAM) wakati kongamano la kujadili namna ya kuendelea kutunz misitu hapa nchini baada ya kumalizika kwa kampeni ya Mama Misitu iliyokuwa inafadhiliwa na Ubalozi wa Finland nchini Tanzania.
 Afisa mradi wa shirika la TRAFFIC, Allen Mgaza akizungumzia kuhusu matokeo ya kazi za Mama Misitu kushirikiana Shirika la WWF wakati wa kufunga kampeni ya Mama Misitu iliyoanza toka mwaka 2008 hadi 2017.
Mratibu wa CBNRM, Jumapili Chenga  kizungumzia namna kampeni ya Mama Misitu ilivyosaidia kupunguza uharibifu wa misitu hapa nchini wakati wa kujadili namna ya kutunza na kusimamia misitu mara baada ya kumalizika kwa kampeni ya Mama Misitu leo Jijini Dar es Salaam
Picha ya Pamoja