CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA VIWANDA VYA MAZAO YA MISITU NCHINI KUTATULIWA

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na  Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIM... thumbnail 1 summary
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na  Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  (kulia) wakati Rais  huyo  alipokuwa  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  ( Picha na Lusungu Helela-MNRT) 
 Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. 
 Baadhi ya  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga  kwenye  kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza  kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  kufungua  kikao cha  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  mara baada   kufungua kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu   nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale inapohitajika kwa kuzishughulikia  changamoto mbalimbali zinazowakabili  ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano  ya Tanzania ya viwanda.
Amesema   Wizara ya Maliasili na Utalii  imedhamiria   kutatua changamoto zinazowakabili  ili kuwawezesha  wamiliki wa viwanda hivyo hasa  wazawa  kutoa  ajira nyingi kwa wananchi.
Amesema  Wizara hiyo haiwezi kufanya kazi pekee yake pasipo  kushirikiana  na sekta binafsi kwani  wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi ambao ndio walinzi wakubwa   misitu nchini.
Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya  viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na  Wawakilishi wa Wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu nchini,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwataka wadau hao  wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao
‘’Nimechaguliwa na Mhe. Rais kuja katika Wizara hii kwa ajili ya kufanya kazi nanyi, tufanye kazi kwa ushirikiano’’ alisema Hasunga
Aidha, Naibu Waziri huyo, amelisema Serikali imeanzisha  utaratibu wa ugawaji wa vitalu   kwa njia  mnada na kwa njia  ya makubaliano binafsi  lengo lake  sio kuviua viwanda  wa mazao ya misitu vya vinavyomilikiwa wazawa bali ni kutaka kila mwenye sifa asiweze kukosa mgao huo.
Akifafanua kuhusiana na utaratibu huo mpya wa   ugawaji wa vitalu ulioanza mwaka jana , Hasunga alisema   asilimi 30 ya vitalu imekuwa ikifanyika  kwa njia ya mnada na asilimi 70 imekuwa ikifanyika kwa njia ya makubaliano binafsi hali iliyopelekea kupunguza malalamiko na pamoja na vitendo vya rushwa kwa wadau.
‘’Kila mmoja wetu hapa atakuwa shahidi hakuna hata mmoja mwenye kiwanda cha mazao ya misitu  aliyekosa mgao  kupitia  huu utaratibu mpya ulianza kutumika mwaka jana’’
Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu juu ya utaratibu huo mpya  ambao wengi ni wazawa kwa kushindwa kushindana na  matajiri lakini hata  hivyo utaratibu huo kwa njia ya mnada   umeisaidia  serikali k kupanga bei  stahiki ya soko katika njia ya makubaliano binafsi.
Hasunga alisema Serikali ipo tayari kupokea mawazo mapya kutoka kwa wamiliki wa viwanda hivyo kama wataona kuna umuhimu wa kuboresha utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu.
Wakati akijibu hoja za wadau hao, Hasunga aliwaagiza waandae ripoti itayoonesha changamoto zinazowakabili na kuiwasilisha ofisini kwake  ifikapo tarehe 10 mwezi ujao kwa ajili ya kufanyiwa kazi
Pia,  Aliwaagiza wamiliki wa viwandao hao kuunda  kitengo  kitakachokuwa na jukumu la  kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo  kujua masoko  pamoja na teknolojia rafiki ya  kuzalisha bidhaa zao zitakanazo na  mazao  ya misitu
Awali, Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus wakati akiwasilisha taarifa yake    ameiomba Wizara  iangalie namna ya kuwasaidia wamiliki wazawa viwanda vya mazao ya misitu  kwa vile  viwanda vilivyo vingi vimeshindwa kujiendesha kutokana na  kukosa malighafi  kwa kuwa wazao hao  wameshindwa kushindana na matajiri wakubwa wakati vitalu vinapouzwa kwa njia ya mnada.
Aliongeza kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) iangalie uwezekano wa kupunguza bei za vitalu hivyo kwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kwa vile bei ya soko la mbao limeporomoka kutokana na  watu binafsi kuuza mbao kwa bei nafuu zilizotokana na miti iliyovunwa  ikiwa michanga.
Naye  Mwenyekiti wa  Chama cha  Umoja wa Wavunaji Sao Hill, Christian Ahiya, ameiomba Wizara kuona uwezekano wa kupunguza tozo 32 zinazotozwa  kwa wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu kwa upande wa wilaya Mufundi  kwa kuwa hali hiyo imekuwa ukiwaumiza na kuwadidimiza.