Watafiti watakiwa kukabiliana na Miti vamizi aina ya MRASHA

Watafiti kutoka nchi ya Tanzania,Kenya na Marekani wakijadiliana jambo kuhusu miti vamizi aina ya Mrasha iliyoko kijiji cha Kahe Wilaya y... thumbnail 1 summary
Watafiti kutoka nchi ya Tanzania,Kenya na Marekani wakijadiliana jambo kuhusu miti vamizi aina ya Mrasha iliyoko kijiji cha Kahe Wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro. Picha na Vero Ignatus
 Mtafiti Dr John Richard Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa misitu  cha Lushoto akifafanua jambo kwa Mtafiti kutoka Marekani. Picha na Vero Ignatus
Mti aina ya Mrasha.Picha na Vero Ignatus Blog.

NA VERO IGNATUS,KILIMANJARO
Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania(TAFORI)kwa kushirikiana na Watafiti wa kutoka wa Kenya,Ethiopia na Afrika ya Kusini wameanza utafiti wa jinsi ya kuangamiza mti vamizi aina ya MRASHA ambao unaharibu uoto wa asili, kilimo, malisho ya mifugo, mifugo yenyewe na binaadamu kwa nchi hizo ikiwemo Namibia

Wananchi wa Kijiji hicho wamewaeleza watafiti hao kuwa baadhi ya madhara wanayoyapata ni pamoja na mifugo yao kufa kutokana na kula mimea hiyo Madhara kwa binadamu ambao wakichomwa na miti hiyo mwilini huota jipu na hata kupoteza baadhi ya viungo mwilini kwa kukatwa ,kuangamiza aina nyingine ya miti

"Hii mimea inamadhara kwetu ukichomwa na mwiba mwilini panaota jipu ,na hili jipu litakuawee hadi linapelekea kupoteza kiungo cha mwili kama ni mkono au mguuni "alisema Ramadhani mkazi wa kijiii cha Ngasini.

" Hii mimea imetapakaa sana huku kwetu na wanyama waliokula mimea hii wamekufa"alisema bi Zahara Yusufu mkazi wa Ngasini.

Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti wa misitu cha Lushoto Dkt.John Richard kilichopo chini TAFORI amesema ,utafiti huo unafanywa kwa majaribio nchini Kenya ,Ethiopia na Tanzania katika kata ya Kahe kijiji cha Ngasini wilaya ya Moshi na misitu Thao ya Mashariki wilaya ya Muheza ambao utatekelezwa kwa miaka sita.

Dkt.Richard amesema hayo baada ya watafiti hao kutoka Nchini Marekani,Swizerland,Uingereza,kutembelea eneo la majaribio ya mradi huo unaofadhiliwa na Swizerland na kufanya majadiliano na wananchi ambao walieleza faida na madhara ya miti hiyo

Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Kenya Purity Rima amesema wananchi wa mji wa Baringo waliwahi kuipeleka Mahakamani Serikali ya nchi hiyo wakidai kulipwa fidia baada ya mifugo yao kupoteza meno kutokana na kula majani ya miti hiyo ambayo nchini Kenya inajulikana kama Mathenge.