SERENGETI WAPINGA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUITWA UWANJA WA KIMATAIFA WA SERENGETI

Mwandishi wetu, Serengeti Mchakato wa kutaka kubadilisha jina la uwanja wa ndege wa Mwanza  kuitwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sere... thumbnail 1 summary


Mwandishi wetu, Serengeti
Mchakato wa kutaka kubadilisha jina la uwanja wa ndege wa Mwanza  kuitwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Serengeti umeingia katika sura mpya baada ya Mbunge wa jimbo la Serengeti Dk Kebwe Steven Kebwe  na uongozi wa halmashauri ya Serengeti kujitokeza katika vyombo vya habari na kuupinga kwa kuwa unalenga kukiuka ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete ya kujenga uwanja wa kimataifa wilayani humo.

Rais Kikwete alitoa ahadi hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 na katika hotuba mbalimbali za mwisho wa mwezi amekuwa akisisitiza juu ya ujenzi wa
uwanja huo katika mji wa Mugumu kwa lengo la kuongeza watalii katika hifadhi ya Serengeti.

Mbunge huyo amesema kitendo cha mkoa wa Mwanza kutaka kutumia jina la serengeti ni dharau kwani mheshimiwa rais aliisha ahidi juu ya ujenzi wa uwanja huo.

Aidha mbunge huyo wa Serengeti ameutaka uongozi wa mkoa wa mwanza kufunga mjadala wa jina la Serengeti na badala yake amewashauri uongozi wa mkoa wa mwanza kuchagua moja ya majina ya viongozi maarufu wa nchi hii na kuwaenzi kwa kuuita uwanja wa ndege wa mwanza.

Naye makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jumanne Kwiro amesema tayari wana hati ya eneo la zaidi ya ekari 5000 kwa ajili ya kazi hiyo na uamuzi wa mkoa wa Mwanza kuanzisha mjadala usio na tija huenda ukamfanya mfadhili aliyekubali kujenga kujitoa .

Mjadala wa jina gani uwanja wa ndege wa Mwanza ulioko katika matengenezo mkubwa ulipamba moto kufuatia Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndukilo kupendekeza kuwa uitwe Serengeti mara baada ya ukarabati wake.