AIR TANZANIA YAFUFUKA TENA, YAREJESHA SAFARI ZAKE KWA KASI, YAJIPANGA KUFANYA SAFARI ZA DUBAI, COMORO.

Tunapenda kuwataarifu kuwa kuanzia Ijumaa, 12 Oktoba 2012, tunarejesha upya huduma zetu za safari ambazo zilisitishwa kwa muda kwa sa... thumbnail 1 summary

Tunapenda kuwataarifu kuwa kuanzia Ijumaa, 12 Oktoba 2012, tunarejesha upya huduma zetu za safari ambazo zilisitishwa kwa muda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

Tunaanza tena safari kati ya Dar es Salaam, Mwanza, na Kilimanjaro siku hiyo, na kupanua wigo wa huduma zetu katika miezi ijayo. Tunatarajia kuanza safari kuelekea Arusha na Zanzibar mwanzoni wa mwezi Novemba, na safari za Mtwara na Moroni Hahaya baadaye mwezi huo.

Tunatarajia kusambaza huduma za safari hadi Dubai kabla ya mwisho wa mwaka.

Tunawashukuru sana nyote kwa uvumilivu wenu na kwa kuendelea kutuunga mkono.

Tafadhali tembelea ofisi zetu au za wakala wa usafiri kufanya booking kwa ajili ya kusafiri na Air Tanzania, The Wings of Kilimanjaro.

Habari hii ni kwa hisani ya page ya Air Tanzania Facebook iliyopostiwa leo Octoba 9, 2012 na kuwekwa hapa na tabianchi blog.