Mwandishi wetu, Dodoma
TAKRIBANI tani 3 za kuni
zinazotumika kwa kila kaya kwa mwaka hazitatumika tena kufuatia Programu ya
uendelezaji Biogesi TanzaniaTDBP kufunga mitambo ya biogesi katika kaya 4500
katika Mikoa 11 nchini.
Mikoa ambayo itanufaika na
mpango huo katika hatua za awali ni pamoja ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Pwani,
Manyara, Dar-es-salaam, Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa na Njombe.
Hayo yamebainishwa na mratibu
wa TDPB lehada Shilla mjini Dodoma katika Mkutano wa kupanga rasimu ya
utekelezaji wa mwaka 2013 uliofanyika Mjini Dodoma kwa lengo la kuboresha
matumizi ya biogesi na hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira.
Wadau wa uendelezaji wa
Biogesi kutoka mikoa mbalimbali wameelezea changamoto wanazokutana
nazo ikiwemo uwezo mdogo wa wananchi kuweza kufungiwa mitambo hiyo.
Mwaka 2013 TDBP imelenga
kufunga mitambo ya Biogesi ipatayo 3300 katika maeneo mbalimbali Nchini hatua
itakayosaidia kukuza uchumi na kuondokana na ukataji miti ovyo unaochangia
athari hasi za tabia nchi.